TIBA MTANDAONI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akisisitiza jambo kwa wataalamu wa sekta ya afya wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma. Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Eng. Peter Ulanga, akiwasilisha mada kuhusu umuhimu wa tiba mtandao nchini kwa wataalamu wa sekta ya afya (hawapo pichani) wakati wa kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma. Kaimu Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Peter Phillip Mwasalyanda (aliyeketi katikati), akisikiliza kwa makini kongamano la ubunifu na utekelezaji wa huduma za tiba mtandao Tanzania ambalo limeandaliwa na UCSAF lililofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa LAPF, Dodoma Wataalamu wa sekta ya afya wakifuatilia kwa makini maelekezo ...