Posts

Showing posts from January, 2018

RC MAKONDA OCTOBER MOSI SHOWROOM ZOTE KUHAMIA KIGAMBONI.

Image
Wafanyabiashara wa Showroom za Magari Dar es salaam wameomba kuongezewa muda wa miezi tisa ili waweze kuhamisha vitu vyao.  Aidha wamefurahishwa na hatua ya serikali kuhamishishia Showroom zote kwenye eneo moja la  Kigamboni na wako tayari kuhama kwakuwa wataongezea ufanisi na idadi ya wateja na mwisho wa siku kuleta ushindani mzuri wa kibiashara kwakuwa serikali ina malengo mema. Ombi hilo limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambapo amewaongezea muda wa miezi tisa na kusema baada ya hapo asiwepo Mtu wa kuomba kuongezwa kwa muda mwingine. RC Makonda ametoa uamuzi huo wakati wa mkutano na wamiliki wa Showroom ambapo amesema ifikapo October mosi showroom zote ziwe zimehamiha Kigamboni. RC Makonda amesema tayari serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu yote muhimu ikiwemo Barabara, Maji, Umeme, Kituo cha Polisi, Madaraja ili wafanyabiashara wafanye biashara kwenye mazingira bora. Amesema faida za uwepo wa showroom kwenye ...

RC WANGABO ATOA MIEZI MITATU KWA WAVUVI ZIWA RUKWA KUHAMA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo ametoa miezi mitatu kwa wananchi wanaoishi katika kambi ya uvuvi ya Nankanga iliyopo kando ya ziwa Rukwa kuhama kwa hiyari baada ya kambi hiyo kuwa katika hatari ya kupatwa na ugonjwa wa kipindupindu kwa kutokuwa na vyoo. Mh. Wangabo amesema kuwa kuondoka huko kwa hiari kuwepo ndani ya mwezi huu wa kwanza hadi wa nne baada ya kuona wingi wa wananchi wanaoishi katika kambi hiyo pamoja na kutokuwepo kwa kipindupindu kwa wakati huu ila zoezi hilo ni la tahadhari ili kujikinga na ugonjwa huo. “Hatuwezi kuendelea kuishi mahali hapa ambapo vyoo vyenyewe vinaingiliana na maji ya kunywa, na ili kisije hapa kipindupindu ni lazima watu wasifanye shughuli kwenye ziwa ili kuwe salama, lakini mkiruhusu kipindupindu kuingia hapa tutawafurusha, tena tutawasimamia kweli kweli, tutawapiga quarantine (kuwaweka kwenye kizuizi) mkipona tutawaswaga,” Amesisitiza Ameyasema hayo alipofanya ziara kwenye kambi ya Nankanga iliyopo katika Kijiji cha S...

NAIBU WAZIRI KANDEGE AVUNJA MKATABA WA TBA.

Image
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe Josephat Kandege akimskiliza Meneja wa TBA Mkoa wa Mara wakati alipotembelea eneo ya ujenzi wa Ofisi za Halmashauri ya Butiama. Hapa ndipo mradi ulipofikia wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama inayojengwa na TBA ambao mkataba wake umesitishwa. Hii ndio Kazi iliyofanyika mpaka sasa kwenye eneo la Ujenzi ilihali taarifa iliyotokewa kwa Waziri Mkuu ni kuwa ujenzi wa Msingi umefikia asilimia 60 Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege ameagiza kuvunjwa kwa Mkataba wa Tsh Bil 3.2 kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama iliyokuwa ikijengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA). Mhe Kandege ameyasema hayo kufuatia Ukaguzi aliyoufanya baada ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyekamilisha ziara yake Mkoani hapa kumuagiza kufanya Ukaguzi huo kutokana na kutoridhishwa na taarifa aliyoipokea kutoka kwa Meneja wa TBA Mkoa wa Mara kuhusiana na mradi huo. Mhe Kandege alisem...

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA MFALME WA DUBAI, WAFANYABIASHARA, ATEMBELEA BANDARI WA JEBEL ALI PORT NA KUTEMBELEA MRADI WA AKHEEL

Image
.   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mwenyeji wake Mfalme Sheikh Mohammed Bin Rashid Al Makthoum, Vice Presdent Prime Minister and Ruler of Dubai, wakielekea katika chumba cha mkutano wakati alipowasili katika makaazi yake Dubai kwa mazungumzo   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akizungumza na Mfalme Shaikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum,Vice President, Prime Minister and Ruler of Dubai, alipofika katika makaazi yake ya kiongozi huo Nchini Dubai akiwa katika ziara yake ya kiserikali, kulia Balozi wa Tanzania katika Nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu UAE Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk na kushoto wasaidizi wa Mfalme, wakiwa katika ukumbi wa mkutano   RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na mazungumzo na Mfalme wa Dubai Shaikh Mohammed Bin Rashid Al Maktoum, Vice President, Prime Minister and Ruler of Dubai, ali...

TRA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA KODI KWA WADAU MBALIMBALI.

Image
 Afisa Muelimishaji Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Rose Mahendeka akiwaelimisha Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi na Mabadiliko ya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2017/18 katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018.   Msaidizi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Chama Siriwa akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Kodi ya Majengo, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018. Meneja wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi toka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bi. Valentine Baltazar akiwasilisha mada mbele ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) kuhusu Taratibu za Kiforodha, katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo 24 Januari, 2018. (PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-TRA). Na: Veronica Kazimoto. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imepongezwa k...

MBUNGE MGIMWA:WATENDAJI KAMATENI WAZAZI WOTE AMBAO HAWAWAPELEKI WATOTO WAO SHULE.

Image
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akizungumza na viongozi wa kata ya Kibengu kuhusu maswala mbalimbali ya kimaendeleo sambamba na kutoa maagizo mbalimbali ambayo yatasaidia kuchochea maendeleo ya kata ya hiyo na jimbo hilo kwa ujumla. Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa na viongozi wengine wakisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Kata ya Kibengu. Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mahamuod Mgimwa akiangalia moja ya mradi wa ujenzi wa vyoo.  Diwani wa kata ya Kibengu Zakayo Kilyenyi akiwa na viongozi wa kata ya hiyo mara baada ya kutoka kwenye kikao na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Na Fredy Mgunda,Mufindi.  Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini amewataka viongozi wa vijiji na kata kuwachukulia hatua za kisheria wazazi wote ambao hawataki kuwapele shule watoto wao wakifaulu mitihani ya shule ya msingi kwenda shule ya sekondari.  Akizungumza na blog hii Mbunge Mahamuod Mgimwa alisema kuwa sa...