RC MAKONDA OCTOBER MOSI SHOWROOM ZOTE KUHAMIA KIGAMBONI.


Wafanyabiashara wa Showroom za Magari Dar es salaam wameomba kuongezewa muda wa miezi tisa ili waweze kuhamisha vitu vyao.

 Aidha wamefurahishwa na hatua ya serikali kuhamishishia Showroom zote kwenye eneo moja la  Kigamboni na wako tayari kuhama kwakuwa wataongezea ufanisi na idadi ya wateja na mwisho wa siku kuleta ushindani mzuri wa kibiashara kwakuwa serikali ina malengo mema.

Ombi hilo limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambapo amewaongezea muda wa miezi tisa na kusema baada ya hapo asiwepo Mtu wa kuomba kuongezwa kwa muda mwingine.


RC Makonda ametoa uamuzi huo wakati wa mkutano na wamiliki wa Showroom ambapo amesema ifikapo October mosi showroom zote ziwe zimehamiha Kigamboni.

RC Makonda amesema tayari serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu yote muhimu ikiwemo Barabara, Maji, Umeme, Kituo cha Polisi, Madaraja ili wafanyabiashara wafanye biashara kwenye mazingira bora.

Amesema faida za uwepo wa showroom kwenye eneo moja ni kupunguza usumbufu kwa wananchi, Mipango miji, ulipaji kodi, kudhibiti wizi wa magari pamoja kuifanya Dar es salaam kuwa soko kubwa la magari Africa.

RC Makonda amesema ndani ya eneo hilo zitapatikana ofisi zote zinazohusiana na biashara za magari ikiwemo TRA, TPA, Bank, Garage, Sheli, Vituo vya polisi, Fire (ones stop center.)

Wafanyabiashara hao wamepatiwa ofa ya kufanya biashara Miaka mitatu kwenye eneo hilo pasipokulipa pamoja na fursa ya kuunganishwa na wauzaji wakubwa wa magari kutoka Dubai kwaajili ya kufanya ubia.

Comments

Popular posts from this blog

ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.

NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

BONANZA LA BAJAJ, BODABODA LAFANA DAR