NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter, akitoa pepo kwa dada huyo aliyekuwa akisumbuliwa na pepo kwenye semina ya maombi iliyofanyika katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa
Rev Joseph Marego.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter, akimuamuru pepo atoke kwa kijana huyo ambaye pepo hilo limemtesa kwa muda mrefu na kumfanya kupoteza kumbukumbu.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter, akiendelea kumuombea kijana huyo aliyekuwa akisumbuliwa na pepo.
Baadhi ya waumini waliohudhuria semina ya maombi iliyofanyika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa
Rev Joseph Marego jijini Dar es Salaam.
Mtumishi wa Mungu Siza Marego akiendelea kuwafungua baadhi ya watu wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwamo mapepo na magonjwa mengine.
Waumini walioshiriki Seimina ya Maombi wakiendelea kufunguliwa wakati Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter akiendelea na mahubiri.
Mtumishi wa Mungu Siza Marego katikati akiendelea kuwaombea watu wenye vifungo mbalimbali.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter, akiendelea kuhubiri katika semina ya maombi iliyofanyika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa
Rev Joseph Marego , jijini Dar es Salaam.
Waumini wakiendelea kufuatilia mafundisho mbalimbali yaliyofundishwa na Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter.
Mke wa Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life, Eliya Peter kushoto na kulia ni Mke wa Rev Joseph Marego wa Kanisa la Tabata Kimanga EAGT, wakiendelea kufuatilia semina hiyo.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter , akiendelea na kuhubiri katika semina hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego.
Kwaajili ya huduma ya Maombi na Maombezi mbalimbali wasiliana na Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life
lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter kwa Namba za Simu:0717 996691 .
ZIJUE FAIDA ZA MAOMBI
1.Utashinda
katika Majaribu au Mateso: Watu wengi hawana muda wa kuomba
ila likitokea jaribu, hulalamika kwa nini limetokea jaribu hilo.
Usipoomba ujiandae kuingia kwenye majaribu na bila
kuomba huwezi kushinda majaribu ya dunia hii.
Kitabu cha Luka 22:
46 ….Akawaambia, mbona mmelala usingizi ? Ondokeni mkaombe msije mkaingia
majaribuni.
Maombi ni kumuita Mungu kama hupendi kumuita Mungu
ujue ujue kuna mateso ya shetani yatakukuta.
Kuna maombi unayotakiwa kuomba ili usiingie majaribuni,
Katika Kitabu cha Zaburi 50:15 ….Ukaniite siku ya Mateso ; Nitakuokoa
, na wewe utanitukuza.
2.Utapokea
Mahitaji yako: Utapokea hitaji lako tu utakapo mueleza
baba yako wa Mbinguni, Katika Kitabu cha Mathayo 7: 7-8 …..Ombeni, nanyi mtapewa, Tafuteni
nanyi mtaona , bisheni nanyi mtafunguliwa.
Lazima ujue faida za maombi na kupokea hitaji lako,
usiseme Mungu anajua haja zangu ila ni lazima ujieleze mbele za Bwana, Katika
Kitabu cha Isaya 43: 26 …Unikumbushe na
tuhojiane, eleza mambo yako upate kupewa haki yako.
3.Utaepuka
mabaya Ibirisi ni kama Simba kila saa anataka kutumeza, Suala
ni Muhimu unapopatikana na mabaya ni muhimu kuomba chochote kinachotokea kwako
ni muhimu kuomba, Katika Kitabu cha
Zaburi 91:10 …. Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.
4.Utafunguliwa
Macho ya Rohoni, Yapo mengi hujayaona ila kupitia maombi
Mungu atakufunulia, Kitabu cha Yeremia 33:3 ….Niite name nitakuitikia, nami
nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
5.
Utaona Ukuu wa Mungu, Tunapoomba kwa bidii Mungu
anajidhihirisha na kutenda mambo makubwa mno tusiyoyategemea, Kitabu cha Yakobo 5:17….Eliya alikuwa mwanadamu mwenye
tabia moja na sisi akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya
nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.
Comments
Post a Comment