RC MAKONDA ATOA KIBALI KWA WASANII.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amepiga marufuku baadhi ya watendaji wanaozuia Wasanii kurekodi Video za Nyimbo au Movie kwenye mandhari (location) mbalimbali za jiji hilo kwakuwa inalorudisha Nyuma Utalii. “Haiwezekani msanii akitaka kurekodi Video au Movie kwenye mitaro ya maji machafu ambayo inatoa taswira mbaya kwa Jiji letu hasumbuliwi vibali lakini akirekodi kwenye Hotel, Majengo Marefu, fukwe au kwenye mazingira mazuri anasumbuliwa kibali, ” alisema RC Makonda na kuongeza “ Hili haliwezekani, kuanzia sasa wasanii mtarekodi Video Location yoyote mnayotaka isipokuwa Ikulu, Mahakama, Maeneo ya jeshi na vituo vya polisi ambapo panahitaji vibali maalumu,” Alisema lengo ni kuona wasanii wanapewa fursa ya kutangaza vivutio vya utalii kupitia kazi za sanaa wafanyazo.