Posts

MATUKIO YA IBADA YA JUMAPILI YA KUWABARIKI WATOTO KATIKA KANISA LA CHRISTIAN LIFE.

Image
  Mtumishi Eliya Peter pamoja na Mchungaji Edward wa Kanisa la Christian Life lililopo Skansa Mji Mpya, Jijini Dar es Salaam  wakimbariki mtoto Myla Chrispine katika Kanisa hilo leo, ikiwa    Ibada ya leo iliambatana na   kubariki watoto na  somo la ibada ya leo ni   NGUVU YA UZAO .   Mtumishi Eliya Peter pamoja na Mchungaji Edward wa Kanisa la Christian Life, wakimbariki mtoto Naomi Jumapili katika Ibada ya leo iliyofanyika kwenye Kanisa hilo.   Mtumishi Eliya Peter pamoja na Mchungaji Edward wa Kanisa la Christian Life , wakimbariki mtoto Clala Emmanuel katika ibada ya leo.   Mtumishi Eliya Peter kushoto  pamoja na Mchungaji Edward  akiita majina ya watoto nane waliobarikiwa leo katika Kanisa hilo.   Mtumishi Eliya Peter pamoja na Mchungaji Edward wa Kanisa la Christian Life wakimbariki mtoto Happya Ndanga katika Ibada ya leo iliyofanyika kwenye Kanisa hilo lililopo Skansa Mji Mpya, nji ya kuelek...

WASICHANA 24,097 WATAPATA CHANJO YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI.

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amezindua zoezi la utoaji wa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi (HPV) ikihusisha Wasichana wenye umri wa Miaka 14. Aidha zoezi hilo litaanza rasmi Jumatatu ya April 23 likihususisha zaidi ya wasichana 24,097 ambao watakaopata chanjo hiyo katika vituo 270 ikiwemo shule na mitaa. RC Makonda amesema utoaji wa chanjo hiyo utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na ugonjwa wa saratani ambao umekuwa ukisababisha vifo vya kinamama wengi  huku akiitaka jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara. Hata  hayo RC Makonda ametoa wito kwa viongozi wa Dini, Madiwani, Wenyeviti wa Mitaa na Wajumbe kuhamasisha jamii kwenda kupata chanjo hiyo. RC Makonda amesema chanzo cha ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi ni pamoja na mapenzi katika umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, kuzaa watoto wengi.  Pamoja na uvutaji wa sigara ambapo dalili zake ni kutokwa na damu bila mpangilio, maumiv...

MASOGANGE AFARIKI DUNIA, MWILI WAHIFADHIWA MUHIMBILI.

Image
  Video Queen maarufu nchini Tanzania,  Agness  Gerald maarufu kama  Masogange amefariki dunia  jioni ya leo Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam. Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili. Hata hivyo Meneja Uhusiano wa wa Hospitali  ya Taifa Muhimbili,   Aminieli Eligaisha amethibitisha kupokea mwili wa marehemu katika hospitali hiyo majira ya saa 12:20 jioni. “Mwili wa Marehemu Agnes  Gerald Masohange tumeupokea  na upo chumba cha kuhifadhia maiti, tumeupokea  majira ya saa 12.  20 jioni hii,” alisema Eligaisha.

TANZANIA KUNADI VIVUTIO VYA UTALII DUNIANI KUPITIA TAMASHA LA URITHI WA UTAMADUNI WA MABARA NCHINI UFARANSA.

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi  Kigwangalla,  Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha la  ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’  Jijini Dar es Saalam jana. ........................................... Tanzania ni miongoni mwa nchi 54 za bara la Afrika zitakazoshiriki katika tamasha la ‘Urithi wa Utamaduni wa Mabara’ linalotarajiwa kufanyika nchini Ufaransa katika mji wa ‘Cherbourg’ mwezi Julai mwaka huu. Tanzania inashiriki tamasha hilo la kihistoria kwa mara ya kwanza ambapo itapata fursa ya kutangaza utamaduni wake na vivutio vya utalii vya mambo ya kale hivyo kuongeza idadi ya watalii na mapato. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha pili cha wadau wa utalii kutoka nchi mbalimbali zinazohusika na tamasha hilo Jijini Dar es Saalam jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi  Kigwangalla, alisema tamasha hilo litatoa fursa pana kwa nchi kutanga...

KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI YA VODACOM YAINGIA UBIA WA KIBIASHARA NA KAMPUNI YA IFLIX.

Image
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa ubia wa kibiashara baina ya iflix na Vodacom. Wateja watapakua apllication ya Playstore au istore ili kupata iflix yenye burudani za Sinema na vipindi vya TV kwa Kupiga *149*01# Kwa sasa kuna vifurushi vya aina tatu, kifurushi cha siku kwa shilingi 1,000, cha wiki kwa shilingi 6,500 cha mwezi kwa shilingi 18,000. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Iflix, Paul Coogan (Kushoto) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia (kulia) wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara wa Vodacom Tanzania Plc, Hisham Hendi (katikati) wakati alipokuwa akiongea kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wak...

SERIKALI YASISITIZA HAKUNA UPOTEVU WA SHILINGI TRILIONI 1.5

Image
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Serikali kuhakikisha kuwa kila kipande cha ardhi hapa nchini kinapimwa ili kuchochea maendeleo wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma.   Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji akitoa taarifa ya Serikali kuhusu hoja ya kutoonekana kwenye matumizi ya Serikali shilingi trilioni 1.51 leo Bungeni mjini Dodoma.   Mbunge wa viti maalum (CCM) Mkoa wa Kagera Mhe. Oliver Semuguruka akichangia hoja ya Bajeti ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kuhusu maboresho yanayopaswa kufanywa katika sekta ya afya ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi katika Mkoa wa Kagera na katika hosipitali zote za umma.   Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni akisisitiza kuhusu mikakati ya Jeshi la Polisi kuendelea kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao kote nchini leo Bungeni mjini Dodoma wakati w...

RAIS DKT MAGUFULI AAPISHA MAJAJI 10, WAKILI MKUU, MANAIBU MWANASHERIA MKUU, MKURUGENZI WA MASHITAKA NA WAKILI MKUU.

Image