MASOGANGE AFARIKI DUNIA, MWILI WAHIFADHIWA MUHIMBILI.
Video Queen maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki
dunia jioni ya leo
Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es
salaam.
Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na
marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii
kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili.
Hata hivyo Meneja Uhusiano wa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminieli Eligaisha amethibitisha kupokea mwili wa marehemu katika hospitali hiyo majira ya saa 12:20 jioni.
“Mwili wa Marehemu Agnes Gerald Masohange tumeupokea na upo chumba cha kuhifadhia maiti, tumeupokea majira ya saa 12. 20 jioni hii,” alisema Eligaisha.
Comments
Post a Comment