MCHUNGAJI MGAMBO ASHAURI SERIKALI KUSIMAMIA MAADILI.
Leonce
Zimbandu
MCHUNGAJI wa
Kanisa la Free Pentecoste (FPCT) Majohe Bwela, David Mgambo ameishauri
serikali kuendelea kusimamia
maadili
bila kubagua vyama vya siasa wala dini ili kuendelea kudumisha amani.
Ushauri huo
umetolewa na Mchungaji Mgambo wakati
wa mahubiri kwenye mkutano wa siku saba wa Injili unaoendelea katika viwanja vya
kanisa hilo wenye lengo la watu wamjue mungu ili kuepuka uovu.
Amesema serikali
hupambana na uhalifu kwa kutumia vyombo vya dola lakini watumishi wa Mungu hushughulikia uovu kwa kuhubiri
neno la Mungu kwa watu wote ili
waachane na uhalifu katika jamii.
“Unajua sisi ni watendakazi wa serikali ya
mbinguni lakini vyombo vya dola
vinafanyakazi kwa kutumia nguvu na
sheria za kidunia, hivyo tukishirikiana tutafanikiwa kutokomeza uhalifu,”
alisema.
Aidha,
Mchungaji Mgambo amesema pamoja na Kanisa
la FPCT kufanya kampeni hiyo Septemba
kila mwaka na lakini yeye alikuwa
akiendelea kumuomba mungu ili
aepushe mauji ya watu wasio na hatia yaliyotokea kule Kibiti, Lindi na Mkurunga.
Aliendelea
kusisitiza kuwa maombi ya watumishi wa Mungu katika matukio yaliyotokea nchini yameisaidia serikali kudhibiti kwa haraka ili kudumisha amani yetu iliyodumu kwa miongo mitano sasa.
Comments
Post a Comment