PROF.KAMUZOLA AHIMIZA UPANDAJI MITI.
KATIBU
Mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mzingira, Profesa Faustin Kamuzola, akizungumza kwenye upandaji wa miti leo jijini Dar es Salaam.
KATIBU
Mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mzingira, Profesa Faustin Kamuzola akiwa kwenye picha na Rais wa Rotary Club of Bahari Dar es Salaam.
KATIBU
Mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mzingira, Profesa Faustin Kamuzola akimwagilia maji baada ya kupanda mti wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.
KATIBU
Mkuu wa ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mzingira, Profesa Faustin Kamuzola akizungumza na viongozi wa Rotary club baada ya kuwasili katika eneo Aga Khan kwenye ufukwe wa Bahari ya Hindi.
Afisa Mazingira wa Manispaa ya Ilala, Feada Magesa akizungumza baada ya mpango wa kupanda miti,kushotokwake ni Rais wa Rotary Club of Bahari Dar es Salaam,Amyn Laljl.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea View, Victor Muneni (anayepiga makofi) akishuhudia mmoja wa vijana wa kikundi cha Mabaharia akiweka udogo kwenye mti aliopanda katika eneo la ufukwe wa Bahari ya Hindi karibu na Hospitali ya Aga Khan.
Leonce Zimbandu
KATIBU Mkuu wa ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mzingira, Profesa Faustin Kamuzola amehimiza watanzania wasiishie
kupanda miti bila kuitunza.
Kauli hiyo imetolewa leo
jijini Dar es Salaam kwenye mradi ya
upandaji miti 200 ulioandaliwa na Rotary Club of Bahari Dar es Salaam kwa kushirikiana na Enviro Care (T) co.Ltd.
Amesema upandaji miti
unamanufaa nchini kwa vile hakuna sekta isiyotegemea miti tangu kuubwa kwa
ulimwengu, ikiwamo sekta ufugaji, misitu, Afya, Utalii na Maji zote zinategemea
uhifadhi wa mazingira.
“Tunawashukuru kwa kujitoa
kwenu kupanda miti 200 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali, endeleeni
na harakati hizo na serikali ipo tayari kutoa msaada kwenu,”alisema.
Amesema mpango wa upandaji
miti upo katika ofisi yao inayoshughulikia mazingira, hivyo wanashukuru kuona
wadau wamejitokeza kusaidia juhudi hizo.
Rais wa Rotary Club of Bahari
Dar es Salaam, Amyn Laljl amesema kuwa club hiyo imejipanga kupanda miti 200
ili kubadilisha Mkoa wa Dar es Salaam
kuwa kijani.
Amesema baada ya kupanda miti hiyo wataendelea
kuitunza kwa muda wa miezi 12 ili kuhakikisha inakua ili kufikia malengo ya kuweka Dar es Salaam
katika hali ya kijani, yakiwamo maeneo ya ufukweni.
“Tutashirikiana na Aga Khan
kwa ajili ya kumwagilia maji miti hiyo hadi
mvua za masika zitakapoanza,” alisema.
Comments
Post a Comment