ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.
ASKOFU MPYA! Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania limemuweka wakfu Mch. Paul Kamau Kabaiya kuwa Askofu wa Kwanza wa Kanisa la Moravian Kenya (The Moravian Church in Kenya) katika ibada iliyofanyika katika Ushirika wa Ruiru, katika County ya Ruiru karibu na Nairobi nchini Kenya jana tarehe 27/11/2017. Ibada ya kumuweka wakfu Askofu Kabaiya iliongozwa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam na Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania, Mhashamu Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula akisaidiwa na Maaskofu wawili wa Kanisa Anglikana la Kiinjili Tanzania ambao ni Mheshimiwa Mhashamu Askofu Kuwayawaya Stephen Kuwayawaya (Mvumi Makulu, Dodoma) na Mhashamu Askofu Edward Wilson (Kibondo, Kigoma) na hivyo kufanya idadi ya Maaskofu waliomuweka wakfu kuwa watatu kama utaratibu na kanuni ya Uaskofu wa mnyororo inavyotaka. Mhashamu Askofu Paul Kamau Kabaiya anakuwa pia ni Askofu Msaidizi wa Dar es Salaam na Askofu wa Kenya. Mhashamu Askofu Kabaiya alisoma Moravian Theological Colle...
Comments
Post a Comment