BONANZA LA BAJAJ, BODABODA LAFANA DAR
Leonce Zimbandu
BONANZA la Madereva wa Bajaji na Pikipiki lililoshirikisha mchezo wa mpira wa miguu limefanyika leo katika viwanja vya Kawe Dar es Salaam na timu ya Afrikana imeibuka kidedea kwa kunyuka timu ya Kawe kwa bao 2-0.
Timu ya Afrikana ilipata nafasi ya kutiga fainali baada ya kuibajua timu, timu ya Mwenge Bajaji kwa goli 1-0 na kuingia fainali moja kwa moja, huku timu Kawe ilianza kwa kuifunga timu ya Masaki kwa mikawaju ya penati bao 5-3.
Kawe iliingia fainali baada ya kucheza nusu fainali na timu ya Mikocheni na kuifuinga bao 2-1 kwa ushindi huo kawe ilijihakikishia kuingia fainali.
Akizungumza katika Bananza hilo Mwenyekiti wa Bananza hilo Wilaya ya Kinondoni, Edward amezipongeza timu zilizoshiriki katika bonanza kwa kuonesha uzalendo wa kupenda michezo.
Amesema kuwa lengo la bonanza hilo ni kubadilishana uzoefu na kufahamiana baina ya timu hizo ili kukuza uhusiano mwema baina yao na kupinga utumiaji wa dawa za kulevya.
“Unajua bonanza hilo limefanyika baada ya kuhudhuria mafunza ya madhara ya kutumia Dawa za Kulevya kwa madereva wanaotumia dawa za kulevya,” alisema.
Amesema katika bonanza hilo mshindi wa kwanza atapata zawadi y ash. 50,000 na mshindi wa pili amezwadiwa sh, 30,000 na kueleza kuwa huo ni mwanzo na wataendelea kuandaa bonanza ili kupata timu ya mkoa.
Nahodha wa timu ya Afrikana, Amiri amesema walifahamu kuwa watakuwa washindi katika bananza hilo hasa kutokana na mazoezi ambayo walikuwa wakichukua.
“Tulistahili kuwa washindi kwani hatujapoteza mchezo wala kufungwa hata goli moja, hivyo naomba bananza lijalo linapaswa kuandali vyema ili timu nyingi zishiriki,” alisema
Vijana walioshiriki kwenye bonaza hilo hivi karibuni wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Baadhi ya vijana wakiwa kwenye maandalizi ya bonaza hilo, hivi karibuni jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadhamini wa bonaza hilo ambao wanatoa mikopo ya Pikipiki na Bajaji kwa vijana lengo ni kuwakwamua kimaendeleo.
Comments
Post a Comment