DIWANI MWENEVYALE AELEZEA JINSI MIRADI YA MAENDELEO ILIVYOTEKELEZWA KWENYE KATA YAKE.
Leonce
Zimbandu
DIWANI wa
Kata ya Majohe, Wazir Mwenevyale amesema katika kipindi cha uongozi wake miradi
mingi ya maendeleo imetekelezwa, ukiwamo mradi wa ujenzi wa kivuko kutoka
Majohe kwenda Kigogo Fresh.
Kivuko hicho
kilianza kujengwa Mei, mwaka huu kwa
gharama ya sh. Milioni 196 ambacho hadi sasa Mkandarasi anasubiri malipo yake
ili kukamilisha ujenzi huo.
Mwenevyale aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii ofisini iliyopo Majohe, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Alisema iwapo mkanadarasi huyo atalipwa pesa yake atakamilisha ujenzi wa mifereji ambayo itasaidia uimara wa kalavati hilo ambalo ni muhimu kwa wakazi wa majohe na vitongoji vyake.
“ Chini ya uongozi wangu ipo miradi mingi imetekelezwa ukiwamo huu a kivuko na kumaliza tatizo la ukosefu wa kivuko katika eneo hilo,” alisema.
Anasema kivuko hicho kimechelewa kutokana mkandarasi kutolipwa malipo yake kwa wakati, hali hiyo imetokana na mfumo wa malipo ya serikali kubadilika lakini suala hilo lipo mbioni kukamilika.
Mkazi wa Majohe, Amina Salehe alisema wamefurahisha na kitendo cha serikali kuwajengea kivuko hicho, kwani walikuwa wakipata shida nyakati za mvua.
“Unajua wanafunzi walikuwa wakipata shida nyakati za mvua na tayari mwananchi mwennzetu alipoteza maisha wakati wa kuvuka ili kwenda upande wa pili, hivyo tunapongeza kwa juhudi zilizofanyika,” alisema.
Comments
Post a Comment