MADEREVA BAJAJI,PIKIPI WAFUNDWA DAWA ZA KULEVYA
Afisa wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Moza Makumbuli, akitoa elimu kuhusu madhara ya madawa ya kulevya kwa madereva hao, leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha
Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi Matatu Tanzania (MAPIMAMATA), Edward Mwenisongole, akitoa ufafanuzi wa mada zilizokuwa zinatolewa kwa madereva hao.
Mkuu wa Kituo cha Kawe, Samson Mwambungu, akiendelea kutoa ufafanuzi kwa madereva hao athari za madawa ya kulevya.
Madereva Bajaji na Pikipiki wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa leo na Afisa kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Afisa Mwendeshaji kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF), Naira Mayage akielezea faida za kujiunga na mfuko huo.
Mwandishi
wetu
MADEREVA wa Bajaji na Pikipiki wa Wilaya ya
Kinondoni wametahadharishwa kutotumia
Dawa za Kulevya ili kujiepusha na ajali
za barabarani zinazochangiwa na makosa ya kibinadamu.
Tahadhari hiyo imetolewa kwenye mafunzo ya siku moja
baada ya takwimu ya kutisha iliyotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
kuwa asilimia 76 ya ajali nchini husababishwa na makosa ya ulevi.
Mtoa mada kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Afisa, Moza
Makumbuli aliyasema hayo alipokuwa akitoa mafunzo kwa madereva hao jijini Dar
es Salaam.
Amesema dawa za kulevya zimekuwa na madhara katika
uendeshaji wa vyombo vya moto, ikiwamo Bangi, Heroin, Mirungi, Cocaine na
Pombe.
“Kamwe usiendeshe chombo cha moto ukiwa umetumia
kilevi, hivyo kila mmoja anapaswaa kujiepusha na matumizi ya dawa hizo ili
kudumisha afya,”alisema.
Alisema pombe huathiri uwezo wa kufikiri,
kutafakari, stamina na uwezo wa kuona
kwa haraka ili kuchukua tahadhari za haraka ili kuepusha ajali kutokea.
Mkuu wa Kituo cha Kawe, Samson Mwambungu alisema
kuwa Dawa za Kulevya hazikubaliki kwa jamii na tishio, hivyo madereva wa vyombo
vya moto wanatakiwa kujiepusha na utumiaji.
“Acheni kutumia dawa za kulevya ambazo ni hatari kwa afya zenu,” alisema.
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki
Matairi Matatu Tanzania (MAPIMAMATA), Edward Mwenisongole amesema mafunzo hayo yamehudhuriwa na madereva
kutoka, vituo mbali mbali, vikiwamo,Msasani, Mwenge,Mlimani City,Kawe,
Africana.
Vingine ni Mwalimu Nyerere,
Tegeta,Mikocheni,Mbuyuni kwa lengo la
kupata elimu ya kujiepusha na matumizi ya Dawa za Kulevya.
Comments
Post a Comment