MADEREVA WAANDAA SEMINA YA KUWAKWAMUA VIJANA NA MADAWA YA KULEVYA.
Na Mwandishi Wetu
MADEREVA Bajaji na Pikipiki wameandaa semina ya wajasiriamali itakayotoa
mafunzo mbalimbali ikiwamo athari ya matumizi ya madawa ya kulevya.
Aidha semina hiyo itakayofanyika Octoba 19
itaambatana na tamasha la michezo litakalofanyika katika viwanja vya Tanganyika
Packers Octoba 22 kuanzia majira ya asubuhi.
Akizungumza na Mwandishi wa Blog hii leo, Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki
Matairi Matatu Tanzania (MAPIMAMATA), Edward Mwenisongole
amesema lengo la semina hiyo ni kutoa elimu kwa vijana kuhusu madawa ya
kulevya kwani wao ni nguvu kazi ya Taifa.
“Kutokana na vijana kuwa nguvu kazi ya Taifa sisi kama viongozi tumeona umuhimu wa kuandaa semina hii itakayo tukutanisha madereva Pikipiki na Bajiji ili kupewa elimu juu ya madawa ya kulevya kwani vijana ndio wahanga wakubwa wa madawa haya,”
Mwenisongole amesema semina ya wajasiriamali na mafunzo kuhusu dawa za kulevya yatafanyika katika ukumbi wa Msasani Club majira ya saa 3:00 asubuhi.
Amesema katika semina hiyo vijana watapata fursa ya Bima ya Afya na kujiunga na Mfuko wa Pesheni (PPF) bure na kupata Mikopo mbalimbali kwaajili ya maendeleo.
Akizungumzia Tamasha la Michezo litakalofanyika katika viwanja vya Tanganyika Packers Octoba 22 amesema tamasha hilo litashirikisha Timu nane kutoka Manispaa ya Kinondoni.
“Tamasha hili la michezo litafanyika kuanzia saa 7:00 asubuhi ambapo timu nane zitashiriki, ikiwamo Combaini ya Kinondoni, Mlimani City, Mikocheni, Mwenge, Masaki, Kawe, Africana, Tegeta na Mbuyuni,”anasema
Comments
Post a Comment