MAKINDA AZINDUA “TOTO AFYA KADI” KWENYE NYUMBA ZA IBADA.
MWENYEKITI
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF )Anne Makinda , akizungumza na baadhi ya waumini baada ya kumaliza uzinduzi wa huduma
ya “TOTO AFYA KADI” leo katika Kanisa la Kanisa
la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe
Mwenge.
MWENYEKITI
wa Bodi ya (NHIF) Anne Makinda, akizungumzia umhimu wa kutumia NHIF wakati wa uzinduzi wa huduma
ya “TOTO AFYA KADI” katika Kanisa
la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe
Mwenge .
MWENYEKITI
wa Bodi ya (NHIF), Anne Makinda akiwasikiliza baadhi ya waumini wa Kanisa hilo ambao walikuwa wakiuliza maswali zaidi kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mfuko huo.
Baadhi ya waumini ambao walitembelea eneo ambalo Maofisa wa NHIF walikuwa wanatoa form kwaajili ya kujaza kwa huduma ya “TOTO AFYA KADI” ambayo imezinduliwa rasmi leo kwenye nyumba za ibada.
Meneja
wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki akiendelea kutoa maelezo ya umhimu ya mfuko huo kwa baadhi ya waumini wa Kanisa la Parokia
ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge.
MA I
Na Mwandishi Wetu.
MWENYEKITI
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), Anne Makinda azindua huduma ya
“TOTO AFYA KADI” kwenye nyumba za ibada
leo.
Akizungumza
na waumini wa Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Maximilian Kolbe Mwenge amesema huduma hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri wa
chini ya miaka 18 kwa Sh. 50,400 kwa
mtoto mmoja kwa mwaka.
Makinda
amesema kampeni hizo ambazo zitaendelea kwenye Madhehebu ya Dini lengo ni kuwa
rafiki na huduma hiyo ili kufikia mwaka kesho watanzania asilimia zaidi ya 80 wawe wamejiunga na huduma hiyo.
Makinda
amesema kiasi hicho cha Sh. 50,400
kitakachochangiwa kwa mwaka kitamuwezesha mwanachama huyo kupata matibabu
katika vituo vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.
Naye Meneja
wa NHIF wa Mkoa wa Kinondoni , Innocent Mauki amesema fao hilo pia hutolewa kwa
wanafunzi wa Shule ya Msingi hadi Chuo Kikuu kwa Sh. 50,400.
Pia amesema
NHIF hutoa huduma kwa vikundi vya
wajasiriamali walio kwenye vikundi vya watu kuanzia 10 kwa Sh.
76,800 kwa kila mwanachama mmoja ambaye
atachangia fedha hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Comments
Post a Comment