MANISPAA ILALA YAVAMIA VIJIWE VYA MATEJA
Mkuu wa Idara ya Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon
Mapunda akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu uhamasishaji na kutoa elimu ya mazingira kwa wananchi.
Wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala na kikundi cha Joging
wakielelea eneo la kufanya usafi Posta ya zamani.
Msemaji
wa Manispaa ya Ilala, Tabu shaibu alikiwajibika kufanya usafi wa mazingira.
Wafanyakazi
wa Manispaa ya Ilala na kikundi cha Joging wakifanya usafi Posta ya zamani eneo
la ufukwe.
MANISPAA Ilala imevamia vijiwe vya Mateja vilivyoko kwenye ufukwe wa Posta ya zamani kwa kufanya usafi wa Mazingira ikiwa ni utekekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli.
Hatua hiyo imechukuliwa na Manispaa hiyo baada ya kubaini kuwa eneo hilo limekithiri kwa taka mchanganyiko, ikiwa viwembe, plastiki, makaratasi na mabaki ya vyakula.
Mkuu wa Idara ya Usafi wa Mazingira Manispaa ya Ilala, Abdon Mapunda aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walioshiriki zoezi hilo jijini Dar es Salaam jana.
Amesema kuwa wananchi wengi wanafirikiria suala la usafi ni jukumu la watumishi wa umma pekee lakini dhana hiyo siyo kweli bali kila mtu anapaswa kufanya usafi katika eneo lake na kuepuka kutupa taka ovyo.
“Tunaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kushiriki kufanya usafi na kutoa ada za uzoaji taka ili kupunguza mlundikano wa taka ngumu katika makazi,” alisema.
Amesema kila wiki usafi hufanyika katika kila Kata bali Manispaa huchukua jukumu la kwenda kufanya usafi kila mwenye katika maeneo korofi, likiwamo ufukwe wa Posta Mpya.
Comments
Post a Comment