MAPIMAMATA WALIOMBA JESHI LA POLISI KUFANYA UKAGUZI.
Na Mwandishi Wetu.
CHAMA cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi Matatu Tanzania
(MAPIMAMATA), kimeliomba Jeshi la Polisi
Nchini kufanya ukaguzi kwenye vituo vya madereva bajaji ili kubaini bajaji
zinazoibiwa.
Akizungumza na mwandishi wa blog hii leo Mwenyekiti wa chama
hicho, Edward Mwenisongole amesema zaidi
ya bajaji 10 zimeibiwa ndani ya mwezi mmoja na madereva wawili kuuwawa na
hakuna hatua yeyote inayochukuliwa.
Mwenisongole, amesema changamoto hii ya kuibiwa hawaoni juhudi yeyote ya kusaidiwa maana wanaamini hizo bajaji zinazoibiwa zinafanya kazi baadhi ya maeneo.
“Tunaliomba Jeshi la Polisi Nchini lifanye ukaguzi kwenye vituo vya madereva wa bajaji ili kubaini bajaji zinazoibiwa hii ni kutokana na wizi unaoendelea na kugharimu maisha yetu,”anasema Mwenisongole
Comments
Post a Comment