MILIONI 800 ZATENGWA ILALA KUJENGA MATUNDU YA VYOO.
Leonce
Zimbandu
MANISPAA ya
Ilala inatarajia kutoa sh. Milioni 65.5
kwa ajili ya ujenzi wa matundu ya choo 16 katika Shule ya msingi Bunge ili kutatua
changamoto ya miundo mbinu
iliyodumu kwa muda mrefu.
Kati ya pesa
tayari sh. Milioni 20 zimetolewa kwa ajili ya kukamilia sakafu ya chini yenye
jumla ya matundu manane na ujenzi wa sakafu hiyo unatarajia kukamilika mwishoni
mwa mwezi huu.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu aliyasema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.
Amesema uamuzi
wa kujenga choo cha ghorofa katika shule ya Msingi Bunge umetokana na hali halisi ya ufinyu wa eneo lenyewe, hivyo serikali
itajenga sakafu mbili, sakafu ya chini matundu manane na juu matundu manane.
“Unajua
juhudi za serikali kutatua changamoto zinaendelea kwa kutenga fedha kila mwaka
kwenye bajeti, kwa mwaka 2017/2018 Manispaa ya Ilala imetenge sh. Milioni 800
kwa ajili ya matundu ya vyoo 400,” alisemaTabu.
Manispaa
imetenga fedha hizo kutoka kwenye vyanzo vyake vya mapato ya ndani na fedha za
maendeleo ya serikali za mitaa (LCDG), pia wadau wanaendelea kuchangia katika
ujenzi wa matundu hayo.
Aidha, Tabu
ameendelea kusema kuwa pamoja matundu yaliyopo ya vyoo laki kutakuwa na chumba
maalumu cha watoto wa kike na walemavu ili kuepusha usumbufu.

Comments
Post a Comment