UTAFITI WA KILIMO KUFANYIKA NCHI NZIMA KUANZIA KESHO.
Mkurugenzi Mkuu wa
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt.
Albina Chuwa akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu
za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo
utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3
Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,
Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo
akihutubia wakati wa kufunga mafunzo ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu
za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo
utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3
Oktoba na kumalizika tarehe 3 Novemba, 2017.
Baadhi ya wadadisi wa Utafiti wa Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 wakifuatilia kwa makini hotuba
ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya utafiti huo mkoani
Dodoma. Utafiti huo wa Takwimu za Kilimo utafanyika nchi nzima kuanzia tarehe 3 Oktoba na kumalizika tarehe 3
Novemba, 2017.

Na Veronica Kazimoto
Serikali kupitia Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) inatarajia kufanya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016/17
nchi nzima kuanzia kesho tarehe 3 Oktoba hadi tarehe 3 Novemba, 2017.
Akizungumza leo wakati wa kufunga
mafunzo ya wadadisi watakaokusanya Takwimu za Kilimo kwa mwaka 2016/17 mkoani
Dodoma, Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Maria Mashingo amesema lengo la utafiti
huo ni kutoa makadirio ya kiasi cha uzalishaji wa mazao makuu, idadi ya mifugo,
mazao yatokanayo na mifugo na maeneo ya kilimo katika mikoa yote ya Tanzania.
"Ningependa
kuwasisitizia washiriki kuwa, dhumuni kubwa la utafiti huu wa kilimo ni kutoa makadirio ya uzalishaji wa
mazao makuu ya kilimo na maeneo yake yaliyolimwa pamoja na taarifa za mifugo
katika mikoa yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania", amesema Dkt.
Mashingo.
Aidha, Katibu
Mkuu huyo ametoa wito kwa wakuu wote wa kaya
watakaochaguliwa kushiriki kwenye utafiti huu, kutoa ushirikiano wa kutosha na
hususan kutoa taarifa sahihi kuhusu hali ya uzalishaji wa mazao, huduma
zinazotolewa na Maafisa Ugani na aina ya mbegu wanazotumia na kubainisha
changamoto wanazokumbana nazo katika shughuli zao za kila siku.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya
Takwimu Dkt. Albina Chuwa amesema jumla ya wadadisi 600 wamepatiwa mafunzo ya
siku 5 kwa ajili ya kufanya utafiti huo nchi nzima.
Dkt. Chuwa amefafanua kuwa
madhumuni ya mafunzo kwa wadadisi hao ni kuwajengea uwezo wa kuhoji na kujaza
madodoso ya wamiliki wa mashamba (wakulima) na namna ya kutambua mahali shamba
lilipo kwa kutumia kifaa maalumu kiitwacho GPS.
Utafiti huu wa Kilimo wa mwaka 2016/17
unafanyika chini ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu,
Zanzibar (OCGS) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara
ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Comments
Post a Comment