ACT- WAZALENDO CHAWAKANA VIJANA WALIOJIUNGA CCM
Mwenyekiti
wa Chama cha ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam Salum Sudi (wa pili kulia)
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukana vijana wane walioamia chama
cha Mapinduzi (CCM) na kujitambulisha kuwa walikuwa viongozi ndani ya ACT
ambapo mwenyekiti huyo alisema siyo
kweli hawakuwa viongozi, kulia ni Katibu Kata ya Kijichi Sadick Mussa (kushoto)
Hassan Mchinya Katibu Mwenyezi Mkoa wa Dar es Salaam na Eliamin Kantu
Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Kijichi (Na Mwandishi wetu)
Na Mwandishi Wetu.
CHAMA cha ACT-Wazalendo,
kimewakana vijana wanne waliojiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), ambapo vijana
hao wakati wakijinadi kwenye mkutano wa Kampeni za Udiwani zilizokuwa
zinafanyika Mwanamtoti Kata ya Kijichi Novemba
12, 2017, walisema kuwa wakati wako ACT walikuwa ni viongozi ambapo chama hicho
kimesema siyo kweli kwamba walikuwa ni viongozi badala yake walikuwa ni
wanachama wa kawaida.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Mkoa wa Dar es
Salaam Salum Sudi, wakati akizungunza na waandishi wa habari Jijini Dar es
Salaam, kuhusu kukana wanachama hao
kwamba siyo kweli kwamba walikuwa ni viongozi.
Mwenyekiti Sudi, aliwataja vijana hao kuwa ni Hassan Massamaki
aliyejitambulisha kama Katibu Kata ya Kijichi, Ally Kera alijitambulisha kama
Mwenyekiti wa Vijana Kata ya Kijichi, Elia Kihoza alijitambulisha kama
Mwenykiti wa Vijana Kata na Kijana Azizi Mukaka alijitambulisha kama
Mhekahazina.
"Hawa vijana ni wahongo, ukweli ni kwamba hawakuwa viongozi ndani ya
ACT-Wazalendo badala yake walikuwa ni wanachama wa kawaida, ifike watu wawe
wanasema ukweli kwani hakuna mtu anayemkataza mwanachama kuamia chama kingine
ni mapenzi ya mtu lakini siyo kwamba mtu aseme uongo ili
kujikweza,"alisema Mwenyekiti Sudi.
Alisema ni vyema baadhi ya watu ambao wanaamua kujiunga na vyama vingine ni
vyema wakachunguzwa kutokana na kwamba wamekuwa wakiviongopea vyama hivyo
kwamba wao waliwahi kushika nyadhifa mbalimbali kumbe siyo kweli.
"Kwa mfano vijana hawa hakuna aliyewahi kuwa kiongozi hata mmoja hivyo
wakati wakijinadi kwenye mkutano wa kampeni walisema kuwa wao walikuwa ni
viongozi kwa nyadhifa mbalimbali kumbe siyo kweli,"alisema Sudi.
Alisema tangu mwaka jana vijana hao walifukuzwa ndani ya chama cha
ACT-Wazalendo walikuwa wanachama awali na si viongozi na wengi wamekuwa
wakilagai sana wakati wakitaka kujiunga na vyama vingine.
Mbali na hilo pia alisema kuwa lipo tatizo la mgombea Udiwani wao Kata ya
Kijichi anayejulikana kwa jina la ..... amekuwa akipata vitisho
mbalimbali ambapo mbali na hilo analiomba Jeshi la Polisi kuingilia kati
kutokana na kwamba mgombea huyo tayari ameisha pata hasara ya kuchomewa shule
yake na kusema kuwa upo umuhimu wa kufanya kampeni za kistarabu tofauti na hali
ilivyo sasa.
Katibu wa ACT-Wazalengo Kata ya Kijichi Sadick Mussa, alisema kuwa wamejipanga
vya kutosha kuhakikisha wanashinda uchaguzi huo na si vinginevyo na kusema kuwa
wananchi wasiwe na wasiwasi kuhusiana na kuibuka kidedea.

Comments
Post a Comment