CHANGAMOTO YA USAFIRI INAVYOKITESA KITUO CHA SIFA.
Mwazirishi wa kituo cha kulelea watoto yatima
cha Sifa Group ambaye pia ni Mwimbaji wa
Nyimbo za Injili Nchini, Sifa John, akielezea jinsi Mungu alivyomuita kwaajili ya kulea watoto yatima ambapo hadi sasa kituo hicho kina watoto 50.
Mtumishi wa Mungu na Mwalimu Alice Haule akizungumza na Mwazirishi wa kituo chicho Sifa John baada ya kuwasili katika kituo hicho kwaajili ya kutoa misaada na kuwafariji watoto hao.
Watoto Yatima wa Kituo cha Sifa Group wakiwakaribisha wageni hawapo pichani waliowatembelea kwaajili ya kutoa misaada mbalimbali pamoja na kuwafaliji.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili na Producer Testimony akiongoza sala kabla ya kuondoka kwenye kituo hicho.
Mtumishi na Mwalimu Alice Haule kulia akiwa na picha ya pamoja na Mwazilishi wa kituo hicho Sifa John kushoto.
Mtumishi na Mwalimu Alice Haule akiwa na familia yake akiwa na picha ya pamoja na Mwazirishi wa kituo hicho.
Mchungaji Mkuu wa Kanisa la Christian
Life Eliya Peter, ambapo miongoni mwa waumini wake waliongozana na familia ya Mtumishi na Mwalimu Alice Haule kwaajili ya kwenda kutoa misaada kwa watoto hao na kuwafaliji.
Mtumishi Mungu na Mwalimu Alice Haule akizungumza na Mwazirishi wa kituo hicho Sifa baada ya kuwasili kituoni hapo jana jioni.
Enles Mbegalo
Mwazirishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha Sifa Group ambaye pia ni Mwimbaji wa Nyimbo za
Injili Nchini, Sifa John, amewaomba watu wenye mioyo ya utoaji na Taasisi mbalimbali kumsaidia kuboresha
miundombinu ya barabara kwenye kituo hicho kilichopo Vikawe Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Hayo aliyasema jana wakati familia ya Mtumishi wa Mungu na Mwalimu Alice Haule
pamoja Muimbaji wa Nyimbo za Injili na Producer Testimony na mke wake na baadhi ya waumini kutoka Kanisa la Christian Life, lililopo Tegeta Nyuki jijini Dar es Salaam, linalosimamiwa na
Mchungaji Mkuu Eliya Peter
waliotembelea kituo hicho na kutoa misaada mbalimbali.
Sifa alisema kutokana na ubovu wa miundombinu
iliyopo kwenye kituo hicho hulazimika kutumia Shilingi 30,000 kwa siku kwaajili ya usafiri.
“Changamoto kubwa iliyopo katika kituo changu ni usafili wa watoto kuwatoa hapa kituoni hadi
shuleni kwani watoto wanasoma Bunju na nalazimika kutoa Shilingi 30,000 kwa siku kwaajili
ya usafili wa gari dogo ambalo tunakodi
kwaajili ya kuwapeleka watoto hawa shuleni na kuwarudisha,” amesema
Hata hivyo alisema changamoto nyingine ni chakula, Sre za Shule pamoja na maji, ingawa tatizo
la maji limetatuliwa kwa kiasi kidogo.
Naye Alice Haule alisema aliguswa na watoto hao na
kumua kwenda kupeleka misaada mbalimbali ikiwamo malazi, chakula na vitu
mbalimbali.
Pia Mtumishi wa Mungu Alice amesema amekuwa akihudumia kituo hicho kwa kipindi cha miaka mitano sasa.
Kwa yeyote atakayeguswa na kutaka kuwasaidia watoto hawa awasiliane na Sifa John kwa namba za simu 0652 562348 na 0766 913780
Pia Mtumishi wa Mungu Alice amesema amekuwa akihudumia kituo hicho kwa kipindi cha miaka mitano sasa.
Kwa yeyote atakayeguswa na kutaka kuwasaidia watoto hawa awasiliane na Sifa John kwa namba za simu 0652 562348 na 0766 913780
Comments
Post a Comment