LUBUVA AIOMBA MANISPAA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA MAENDELEO YA MTAA NA SIO KULETA VITISHO.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa
Oysterbay, Zefrin Lubuva, aliyeshika mdomo akiwa na vijana wa ulinzi na shirikishi kwenye mtaa wake, wakiangalia ofisi ambayo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imeweka alama ya X baada ya kuanza ujenzi wa ofisi ya kudumu kwenye mtaa huo.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa
Oysterbay, Zefrin Lubuva, aliyevaa suti ya kaki akiwa na baadhi ya vijana wa ulinzi shirikishi mbele ya ofisi ambayo inajengwa kwenye mtaa huu.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa
Oysterbay, Zefrin Lubuva akitoa maagizo kwa vijana wa Ulinzi Shirikishi kuimarisha ulinzi kwenye eneo ambalo ofisi imejengwa.
Baadhi ya vijana wa Ulinzi Shirikishi wakiwa wamesimama kwenye ofisi ya Serikali ya Mtaa inayoendele kujengwa.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa
Oysterbay, Zefrin Lubuva, akiwa na baadhi ya vijana wa Ulinzi Shirikishi wakiimarisha ulinzi kwenye ofisi inayojengwa kwa nguvu za wananchi huku Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ikiwataka kuondoa ofisi hiyo.
Na Mwandishi
Wetu.
MWENYEKITI
wa Serikali ya Mtaa Oysterbay, Zefrin Lubuva, ameiomba Halmashauri ya Manispaa
ya Kinondoni kutoa ushirikiano kwenye juhudi za maendeleo zinazofanywa na nguvu
ya wananchi kwenye mtaa badala ya kutoa vitisho.
Ombi hilo amelitoa leo jijini Dar es Salaam, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa ofisi unaoendelea kwenye
mtaa wake ambapo Maofisa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni wametaka
ujenzi huo kutoendelea.
“Eneo hili la
wazi la makutano ya barabara ya Karume
na Msasani liliainishwa tangu 2014 kuwa ni eneo ambalo litajengwa ofisi ya Mtaa
na Halmashauri walileta kontena hili ambalo tumeanza kujengea ofisi hii,”anasema
Lubuva na Kuongeza
“ Mimi baada ya kuingia madarakani 2015 niliona ni
bora nianze ujenzi huu wa ofisi ya kudumu, ila cha kushangaza baada ya serikali
ya mtaa kuanza ujenzi huu kwa nguvu za
wananchi eneo ambalo Halmashauri waliweka kontena hili wamekuja kuweka alama ya
X na kututaka tuondoe ofisi hii,”
Lubuva anasema wakati walipoanza kujenga ofisi hiyo
alifuata taratibu zote na aliandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Kinondoni na Meya kutoa taarifa za ujenzi huo.
“Ofisi hii sijaanza kukurupuka kujenga nilitoa
taarifa, na ofisi hii sio yangu ni ofisi
ya mtaa na wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo ndio waliochangia ujenzi huu, wakati ujenzi
wa ofisi ya mtaa ni jukumu la Halmashauri,”
Pia aliiomba Halmashauri kuacha zama za ukandamijazi
kwani Mamlaka za mitaa zinabeba majukumu makubwa hivyo Halmashauri inapaswa
kuziunga mkono.
Hata hivyo mwandishi wa
blog hii alimtafuta Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni Alon Kagulumjuni
ili aweze kulitolea ufafanuzi suala hilo simu yake ya mkononi iliiita
bila kupokelewa.
Comments
Post a Comment