MAELFU YA WAKAZI DAR WATUMIA IPASAVYI FURSA YA RC MAKONDA YA UPIMAJI NA MATIBABU BURE NDANI YA MELI YA CHINA.

*Maelfu
ya Wananchi wa Dar es Salaam Leo wamejitokeza kwa wingi* kuchangamkia fursa ya
*Upimaji na Matibabu Bure ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya China* ambapo
katika Hali isiyotarajiwa wananchi kutoka *Mikoani na Nje ya Jumuiya ya Africa
Mashariki wamesafiri kuja kufuata huduma hiyo.*
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam
*Mhe. PAUL MAKONDA* amewatembelea wananchi hao na kusema *kila atakaefika na
kupatiwa kadi atapatiwa vipimo, matibabu na dawa Bure* na kuwaasa wananchi kutumia
vyema fursa hiyo.

*RC MAKONDA* amesema Madaktari wengine wa China wanaendelea na huduma za matibabu kwenye *Hospital za Muhimbili, MOI, Ocean Road, Mwananyamala, Amana na Temeke* ili kuhakikisha wanahudumia idadi kubwa ya wananchi.
Amesema *hadi kufikia majira ya mchana tayari wagonjwa 516 walikuwa wamepimwa na kupatiwa matibabu* jambo linaloonyesha kuwa wananchi wote watapatiwa huduma.

*MAKONDA* amesema *wapo madaktari bingwa maalumu waliobobea kwa kutoa dawa za kichina* kwa wale wagonjwa ambao dawa nyingine zimekuwa zikishindwa kutibu.
Amesema lengo ni kuhakikisha *hakuna mtu anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma au kumudu gharama.*




Comments
Post a Comment