MKIKITA WASAINI MKATABA NA FARMSTER YA ISRAEL KUTAFUTA MASOKO YA MAZAO YA MKULIMA KWA MTANDAO WA SIMU

 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson wakitia sahihi mkataba wa makubaliano ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu. Hafla hiyo ilifanyika viwanja vya Camp of Good Hope, Goba  jijini Dar es Salaam.

Abramson ambaye ni mwasisi wa Farmster aliwaelezea waalikwa waliofika kwenye hafla hiyo jinsi  jinsi ya kujiunga na mtandao huo kwa kutumia simu za smart na za kawaida yaani 'vitochi' ambapo mkulima huingiza namba ya simu 0623 753016 kwa kutuma neno Jambo.

Mkulima atapaswa kutaja jina lake, eneo analoishi yaani shamba lilipo, analima zao gani, heka ngapi na anatarajia kuvuna lini na kwa kiasi gani ambapo huunganishwa moja kwa moja kwa mteja atakayejadiliana bei ya kuuzia.

Wakala Mkuu kati ya Mkulima na Mnunuzi utakuwa ni Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (MKIKITA), kitendo ambacho kitasaidia sana kuuvunja mtandao wa madadali wanaosumbua na kuwaibia wakulima.

Wakulima waliohudhuria hafla hiyo walionekana kufurahishwa na ujio wa teknolojia hiyo mpya na ya kisasa itakayowarahisishia wakulima kupata masoko mazao yakiwa shambani.IMEANDALIWA NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Adam Ngamange (kushoto) akibadilishana hati za makubalino baada ya kutiliana sahihi mkataba  na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu.

 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao wa Kijani Kibichi Tanzania (Mkikita), Dk. Kissui S. Kissui (kushoto), akimpongeza Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Farmster ya Israel, Adam Abramson kutiliana sahihi mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi Mtendaji wa  Mkikita, Adam Ngamange (katikati) ambapo Farmster itatoa huduma za upatikanaji wa masoko ya mazao na bidhaa za wakulima wanachama wa Mkikita kwa njia ya mtandao wa simu. 

 Abramson akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo

 Akionesha namba ya kujiunga na mtandao huo


 Wanachama wa Mkikita wakisikiliza wakati mtalaamu huyo akiwaelezea faida mbalimbali atakazopata mkulima kwa kutumia mtandao huo.

 Abramson akionesha eneo alipo mmoja wa wakulima aliyejiunga na mtandao huo.

 Mkulima akipata maelezo kutoka kwa Abramson.

Comments

Popular posts from this blog

ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.

NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA MFALME WA DUBAI, WAFANYABIASHARA, ATEMBELEA BANDARI WA JEBEL ALI PORT NA KUTEMBELEA MRADI WA AKHEEL