MOROVIANI UKONGA YAJIPANGA KUJENGA MAADILI KWA VIJANA
Goodluck Michael akibatizwa katika ibada ya Jumapili jana,
katika kanisa la Morovian Ukonga .
Ibada ya ubatizo na kipaimara ikiendelea katika kanisa la Moroviani Ukonga iliyofanyija jana.
Kwaya ya Ustawi wa Jamii wakitumbuiza kwenye ibada hiyo jana.
Mwandishi wa Habarai wa Upendo Radio Michael Malanyi akiwa
kwenye picha ya pamoja na familia yake baada ya ibada .
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Morovian Ukonga , Samweli
Mwambopo kulia na Wachungaji wenzake
wakizungumza na waandishi wa habari
baada ya kumaliza ibada ya jana.
Michael
Malanyingi
MCHUNGAJI
Kiongozi wa Kanisa la Moraviani Ushirika wa Ukonga, Samwel Mwambopa amesema
Kanisa limejipanga kuwajengea uwezo
vijana kwa kuwafundisha maadili ya kikristo, yakiwamo mafundisho ya
ubatizo na kipaimara.
Kauli hiyo imetolewa
na Mchungaji huyo kwenye ibada ya ubatizo na kipaimara iliyofanyika katika
Kanisa hilo mwishoni mwa wiki jijini Dar
es Salaam.
Alisema mafundisho ya vijana hao 20 yalitolewa kwa
muda wa mwaka mmoja kwa lengo la kuwajenga na kuimarisha kiimani ya kikristo
ili kulinda maadili ambayo yapo hatarini kutoroka.
“Unajua vita
dhidi ya ufisadi ni matokeo ya mmomonyoko wa maadili, hivyo tunahitaji
kurudisha maadili kwa vijana ili kukomesha vitendo hivyo,” alisema.
Alisema
kanisa, wazazi na walezi wanaendelea kujipanga kuhakikisha elimu iliyotolewa kwa vijana hao
inaendelezwa na kudumisha maadili mema katika jamii na Taifa kwa ujumla.
Mchungaji wa
Kanisa la Sayuni toka Boko ambaye aliongoza ibada hiyo ya Kipaimara, Mwigane
Mwakalinga alisema iwapo maadili hayo yataendelezwa, usanii ndani ya kanisa
utaondoka.
Alisema kila
mkristo anapaswa kujiandaa kabla hajafika kwenye madhabahu ya mungu kwa vile
anapatikana kwenye sifa, hivyo hata waimbaji wa nyimbo za injili wanapaswa
kujiandaa na kuonesha heshima mbele ya
madhabahu.
“Unajua
waimbaji wengi hujisahau wanapotoa huduma ya uimbaji kwenye madhabahu,
wanatakiwa kujiandaa na kunyenyekea wakati wa kutoa huduma,” alisema.
Aliongeza
kuwa wengi wanabadilisha hata staili ya nywele zao na hata mavazi yao, hivyo
kanisa litahakikisha usanii wa aina hiyo unarekebishwa ili kufuata maadili ya
kanisa na siyo ya kisanii.
Mmoja wa
wazazi wa watoto waliopata ubatizo,Amisa Joseph alisema kuwa yeye kama mzazi wa
Goodluck Michael atahakikisha mtoto wake
anaendelea kukua katika maadili mema.
“Tunaendelea
kumwomba mungu atusaidie ili kulea familia yetu katika njia ziwapasazo za
kikristo,” alisema.
Comments
Post a Comment