RC MAKONDA AANDIKA HISTORIA, MELI KUBWA YENYE HOSPITAL NDANI YAWASILI NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CHINA.
Meli kubwa ya Jeshi la
Jamuhuri ya China yenye Hospital ndani imewasili
Leo ikiwa na Madaktari Bingwa 381,Vifaa na Madawa ya kutosha kwaajili ya kuanza
kwa zoezi la Upimaji na Matibabu Bure kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Mhe. PAUL MAKONDA ametembelea Meli hiyo na kujionea namna imesheheni Vifaa tiba
vya Kisasa ambapo ndani yake vipo vyumba 8 vya Upasuaji, Vyumba vya ICU, Wodi
za Wagonjwa, Vyumba vya Madaktari, Mitambo ya kisasa, Mahabara na Sehemu ya
Wagonjwa kupumzika.
Meli hiyo ya kipekee ina Helicopter kwaajili ya wagonjwa ambapo kwa Ulimwenguni Meli za Aina hiyo zipo Mbili pekee ambapo moja ni hii iliyokuja Tanzania na nyingine ipo Nchini Marekani.
RC MAKONDA amesema Meli hiyo ina mfumo maalumu wa Mawasiliano Kati ya Meli na Taifa la China pale inapotokea Ugonjwa umeshindikana.
Tayari Jopo la wataalamu 30 wameenda Hospital za Amana, Temeke, Mwananyamala na Ocean Road kwaajili ya kukarabati na kufunga vifaa vipya kwa vile vitakavyobainika vilivyoharibika au Kufa.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha kukosa huduma.
Amewasihi Wananchi wenye magonjwa yaliyoshindikana kwa muda mrefu kuchangamkia Fursa hii ya matibabu Bure chini ya Madaktari Bingwa kutoka China.

Kwa upande wake kiongozi Mkuu wa Meli hiyo Kamanda GUAN BAILIN amesema wamekuja na vifaa vya kutosha na madaktari waliobobea hivyo wananchi Wajitokeze kwa wingi.






Comments
Post a Comment