RC MAKONDA ATANGAZA VITA NA WANAUME WANAOTELEKEZA WATOTO.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa PAUL MAKONDA Leo ametangaza kiama kwa
Wanaume wenye michezo ya kuwazalisha Wanawake kisha kuingia mitini kwa kukwepa
majukumu ya kulea mtoto jambo linalosababisha ongezeko la Watoto wa Mitaani na
ombaomba.
Mheshimiwa MAKONDA amesema
anataka kuongezea nguvu Idara ya Ustawi wa Jamii kwa kuuunda kamati ya Wanasheria
Wabobezi kwaajili ya kuwapeleka Mahakamani Wanaume wanaotelekeza Familia na
kuwaachia Wanawake mzigo wa Malezi.
Aidha amesema kuwa Kamati
hiyo pia itafanya Marekebisho ya Sheria ya pesa ya matunzo ya mwezi Kwa Mtoto
kisha kuwasilishwa Bungeni kwakuwa pesa inayotolewa ni ndogo na haiendani na
maisha ya sasa.
Amesema ni lazima ifike
Mahala Mwanaume anaposababisha Ujauzito kwa Binti atambue analojukumu la
kuhudumia.
RC MAKONDA amesema hayo
wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi za Vifaa vya Ultrasound 10 za kisasa Aina
ya "GE Vscan Access" zenye thamani ya zaidi ya shilingi Million 150
kwa Hospital 10 zilizofanya vizuri katika kutoa huduma bora za Afya na kupunguza
vifo vya Mama na Mtoto wakati wa kujifungua.
Amezipongeza Hospital,
Zahanati na Vituo vya Afya vilivyofanikisha Mkoa wa Dar es Salaam kuwa kinara
wa huduma bora za Afya na Kupunguza Vifo vya Mama na Mtoto na kuwaasa Watoa
huduma kuwa na lugha nzuri kwa Wagonjwa.
Kwa Upande wake Mshauri
Mtaalamu wa Magonjwa ya Mama na Mtoto kutoka CRDB Dr BRENDA DIMELLO amesema Dar
es Salaam imekuwa Mkoa wa kwanza kupunguza vifo vya Mama na Mtoto kutokana na
usimamizi thabiti wa RC MAKONDA na watendaji wa Afya.

Comments
Post a Comment