RC MAKONDA ATEMBELEA OFISI ZA CLOUDS MEDIA GROUP.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe. PAUL MAKONDA* leo ameambatana na *Kamati ya Ulinzi na Usalama* kutembelea na kutoa Pole kwa *Kituo cha Utangazaji cha Clouds Media Group* kufuatia Sehemu ya *Studio za kituo hicho kuungua Moto*. 

*RC MAKONDA* amewapa pole *Viongozi na Wafanyakazi* wa Kituo hicho kwa *taharuki na hasara* iliyotokana na Moto huo. 

Aidha *MAKONDA*amepongeza Jeshi la Zima Moto na Uokoaji kwa *kufika eneo la tukio kwa Wakati* na kufanikiwa kuzima Moto huo ambapo ameliasa *Jeshi hilo kuendeleza Weledi huohuo hata kwa Wananchi*. 
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Clouds Media Group Bwana *JOSEPH KUSAGA* amemshukuru *RC MAKONDA* na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa Ushirikiano Mshikamano walioonyesha. 

*Kwa Mujibu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji imebainika kuwa Chanzo cha Moto huo kilitokana Hitilafu ya Umeme kwenye Chumba ambacho kilikuwa hakitumiki.*

Comments

Popular posts from this blog

ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.

NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA MFALME WA DUBAI, WAFANYABIASHARA, ATEMBELEA BANDARI WA JEBEL ALI PORT NA KUTEMBELEA MRADI WA AKHEEL