*RC MAKONDA AWEKA UTARATIBU WA KUWAHUDUMIA WALIOFANYIWA UPASUAJI NDANI YA MELI*
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam *Mhe.PAUL MAKONDA* amesema Serikali inaweka *utaratibu
wa kuendelea kuwahudumia Wagonjwa waliotibiwa ndani ya Meli ya Jeshi la China
pindi Meli hiyo itakapoondoka* wakiwemo wale waliofanyiwa *Upasuaji* na
kuonekana wanahitajika kuendelea kupewa Matibabu hadi hapo watakapopona.
*RC MAKONDA* amesema kundi la
Pili litakalohudumiwa ni *Wale waliopatiwa matibabu lakini kuna Dawa watatakiwa
kuendelea kuzipata* Serikali itaweka utaratibu wa kuendelea kutoa *Dawa hizo
Bure* hadi wapone.
Aidha *RC MAKONDA* amesema
*watu wote waliopatiwa Namba za Matibabu watahudumiwa pasipo usumbufu wowote.*
Amesema *idadi kubwa ya watu
waliojitokeza kupima Afya haimaanishi kwamba Watanzania ni wagonjwa* Bali ni
mwitikio wa watu kutoka mikoani na nje ya Nchi waliofuata huduma hiyo.
Lengo la Serikali kutoa
huduma ya Matibabu Bure ni *kuwawezesha wasiokuwa na kipato kuweza kupata
matibabu* ili kuhakikisha Hakuna mwananchi anaepoteza maisha kwa kigezo cha
kutomudu gharama za matibabu.
*Ameishukuru Serikali ya
China kwa upendo walioonyesha kwa Wagonjwa waliokwenda kutibiwa Bure* Hali
inayodhihirisha Ukomavu wa Mahusiano baina ya Tanzania na China.
Comments
Post a Comment