RC MAKONDA, WAGONJWA WENYEHALI MBAYA KUSAFIRISHWA NCHINI CHINA NA KUTIBIWA BURE.
Zoezi
la Upimaji wa Afya na Matibabu Bure Ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya Watu
wa China Leo limeingia Siku ya Pili ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.
PAUL MAKONDA amesema Wagonjwa ambao wataonekana kuwa na Hali mbaya watasafirishwa
kutibiwa Bure Nchini China.
MAKONDA amesema kasi ya utoaji wa huduma ni nzuri hivyo anaamini hadi siku ya Mwisho ya Zoezi la Upimaji Wananchi wote waliopatiwa namba watakuwa wamehudumiwa.


RC MAKONDA amesema Ofisi yake
itaratibu utaratibu wa Hati za Kusafiria (Passport) ili kuhakikisha Wagonjwa
wanapatiwa Matibabu ili kuokoa Maisha yao.
Aidha amesema Wagonjwa Wanaopangiwa kulazwa kwenye Meli hiyo yenye Vitanda vya Wagonjwa zaidi ya 300 wanapatiwa huduma za Malazi bure ikiwemo Chakula, Vinywaji, Mavazi.
Aidha RC MAKONDA amekemea tabia ya baadhi ya Watu wanaochuchuwa Kadi za Matibabu kisha kuziuza kwa Watu.
Katika kuongeza nguvu kasi ya Upimaji Madaktari kutoka JWTZ, Muhimbili na Hospital za mkoa wa Dar es salaam Ikiwemo Amana, Temeke na Mwananyamala wanashirikiana na Madaktari wa China katika kutoa huduma.





Comments
Post a Comment