VIJANA CHANGAMKIENI FURSA ZINAZOTOLEWA NA SERIKALI.
Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilaya ya
Kinondoni ambaye pia ni Mshauri wa chama
cha Madereva hao, David Massatu akizungumza na madereva hao baada ya kuwasili kwenye semina hiyo.
Meza kuu wakifuatilia mmoja wa Maofisa kutoka Kampuni ya Bajaji ya Sunbeam Auto, inayotoa mikopo ya bajaji Mpya aina ya RE 4S kwa gharama nafuu, katikati ni Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilaya ya Kinondoni ambaye pia ni Mshauri wa chama cha Madereva hao, David Massatu, kulia ni Ofisa Maendeleo
ya Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Masalida Zephania Njashi na kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki
Matairi Matatu Tanzania (Mapimamata), Edward Mwenisongole.
Baadhi ya madereva Bajaji wakifuatilia semina hiyo ya fursa mbalimbali kwa vijana leo jijini Dar es Salaam.
Madereva hao wakiendelea kufuatilia mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwenye semina hiyo leo.
Mmoja wa maofisa kutoka Kampuni ya Bajaji ya Sunbeam Auto, inayotoa mikopo
ya bajaji Mpya aina ya RE 4S, akitoa ufafanuzi juu ya mikopo inayotolewa na Kampuni hiyo.
Na Mwandishi Wetu.
OFISA Maendeleo
ya Vijana Mkoa wa Dar es Salaam, Masalida Zephania Njashi amewataka
vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa
na Serikali ili waweze kujikwamua kimaendeleo.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati
akifungua semina ya siku moja ya kutoa
elimu kwa madereva wa Bajaji Kituo cha Ukwamani juu ya fursa za vijana zinazotolewa na serikali.
“Serikali hasa hii ya awamu ya Tano ya Rais John
Pombe Magufuli imekuwa ikitoa fursa
nyingi kwa vijana lakini vijana wamekuwa hawatumii fursa hizi kwa kuwa hawapo
kwenye makundi yaliyosajiliwa,”amesema
Aidha aliwataka vijana hao kujiunga katika makundi
mbalimbali kupitia Chama Cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki Matairi Matatu Tanzania
(MAPIMAMATA) ili waweze kujisajiri na
kupata mikopo kupitia vikundi hivyo kwani wakisajiliwa na kutambulika kisheria
ni rahisi kupata mikopo.
Hata hivyo aliwaomba
madereva hao kuisaidie serikali
kupaza sauti kuhusu matukio mbalimbali ya uharifu ambayo yamekuwa yakitokea kwani wao kutokana
na huduma wanayoitoa ni rahisi kuwatambua watu hao.
Kawa upande wake Kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi ( UVCCM) Wilaya ya
Kinondoni ambaye pia ni Mshauri wa chama
cha Madereva hao, David Massatu amesema maendeleo ya Mkoa wa Dar es Salaam
yanawategemea vijana kwani wao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Pia alisema atawakutanisha madereva hao na Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ili aweze kutambua huduma wanazozitoa na
kuwapa ushirikiano.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo ya Madereva Pikipiki
Matairi Matatu Tanzania (Mapimamata), Edward Mwenisongole amesema viongozi wa vyama vya siasa wamekuwa
wakiwajengea chuki vijana na serikali kwani wao wamekuwa wakitetea maslahi yao tu.
“Viongozi wa siasa wamekuwa hawazungumzii fursa
zinazotolewa na serikali kwa vijana ila wamekuwa wakitetea maslahi yao tu, hizi
fursa zilizopo serikalini wanasiasa wamekuwa hawatuelezi zaidi ya kutujengee chuki tu,”amesema
Hata hivyo semina hiyo iliambatana na utoaji wa
elimu kwa vijana na kujitambua na kutoa fursa ya mikopo ya gharama nafuu kwa
Kampuni ya Bajaji ya Sunbeam Auto, inayotoa mikopo ya bajaji Mpya aina ya RE 4S.
Comments
Post a Comment