WAITARA AIPIGA MKWARA CCM KIVULE.
Mwenyekiti wa CCM
Ilala, Ubaya Chuma akimdadi mgombea wa chama hicho Amos Angaya kwenye uzinduzi wa kampeni kivule, mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa CCM toka mitaa mbali mbali, waliohudhuria kampeni hizo mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wanachama waliohudhuria kwenye kampeni hizo.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga akimnadi mgombea wa chadema Nasoro
Bihimba.
Baadhi ya wanachama wa Chadema waliohudhuria kwenye kampeni hizo mwishoni mwa wiki.
Tambwe Hiza akizungumza na wanachama wa Chadema hawapo
pichani.
Leonce
Zimbandu
TAMBO za uchaguzi mdogo wa wenyeviti wa mitaa katika Kata ya Kivule Jimbo la Ukonga
zimeanza kutawala huku Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakihitaji kuurudisha mtaa huo
mikononi mwao na Chadema wakihitaji
kuendelea kuushikilia.
Akizungumza wakati
wa kuzindua kampeni hiyo mwishoni mwa wiki kwenye standi ya Mbondole,
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma alisema kuwa watahakikisha
wanarudisha heshima kwa kushinda uchaguzi huo.
Alisema
wanachama wa CCM wanatakiwa kujiuliza kwa nini mtaa huo ulichukuliwa na
Chadema, hivyo jibu likipatikana itakuwa rahisi kwao kutwaa ushindi mapema.
“Tumejipanga
na timu yetu ya ushindi, hivyo letu tumezindua kampeni na kuwanadi wagombea wa
mitaa mitatu na kuwaombea kura,” alisema.
Wakati CCM
wakiendelea na tambo hizo, Mbunge wa
jimbo la Ukonga Mwita Waitara amewaasa wananchi na wanachama kufanya kampeni za kistaarabu na kamwe
wasikubali kutumika vibaya.
Alisema
hataki vurugu itokee katika jimbo hilo kwenye uchanguzi wa wenyeviti wa mitaa
mitatu ya Kata ya Kivule, ukiwamo mtaa wake wa kivule kati.
Mitaa
mingine ni Bomba mbili, Kerezange huku Mtaa wa Magole ukisubiri uhakiki wa
mipaka ili kubainisha wananchi hao wako Temeke au Manispaa ya Ilala.
“CCM
wanapaswa kufanya kampeni za kistaarabu kwa vile jimbo na kata ya Kivule
linaongozwa na Chadema, hivyo wanapaswa kuheshimu sheria na kanuni,” alisema.
Alisema CCM
wanatoa ahadi ambazo wanataraji kuzifanya lakini Chadema ndani ya miaka miwili
wanazungumzia mafanikio katika jimbo na mitaa mbali mbali.
Comments
Post a Comment