BONDIA ALIYENYIMWA VIZA KAANDAA PAMBANO.
Bondia Shaban Madilu kushoto wa Mtaa wa Mbondole Kata ya Msongola anatarajia kupanda ulingoni Kesho kupambana na Bondia Kutoka mkoani Tanga Patrick Kimweri. Leonce Zimbandu MBONDIA Shaban Madilu wa Mtaa wa Mbondole Manispaa ya Ilala ameamua kuandaa pambano la ngumi la raundi 10 la baada ya kunyimwa visa ya miezi sita kwenda nchini Uingereza. Lengo la Bondia huyo kuandaa pambano hilo ni kuukaribisha mwaka 2018 na kujitanga kuwa bado yupo kwenye ulingo wa masumbwi hiyo anahitaji serikali kumsaidia ili kuondokana na ukiritiba. Madilu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa kupima uzito kwa ajili ya pambano la kesho mwaka mpya kati yake na Bondia kutoka Tanga Patick Kimweri. Anasema baada ya kukosa visa hiyo hakukata tamaa, hivyo aliendelea na mazoezi hadi kufikia wakati huu wa kuandaa pambano lake mwenyewe ili serikali itambue kuwa hata pembezoni ya Jiji wapo wanamichezo. Bon...