MCHUNGAJI AOMBA USHIRIKIANO SERIKALINI.
Leonce
Zimbandu
SERIKALI
imeobwa kuendelea kushirikiana na mashirika ya dini ili kuweka utayari wa
kupambana na mabaya ambayo yanaweza kujitokeza dhidi ya Taifa na kuepuka
kunyosheana vidole.
Ombi hilo
limetolewa kufuatia serikali siku za
hivi karibuni kuwatuhumu viongozi wa dini kuwa wanaingilia masuala ya siasa
badala ya kushughulikia wito wao wa kumtumikia Mungu.
Mchungaji wa
Kanisa la Pentecostal Assemblies of God (PAG) Yombo Vituka, Stanley Uloni aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Alisema
watukio mengi yaliyotokea nchini yanasababishwa na watu kushindwa kumtegemea
mungu katika shughuli zao na kupoteza upendo miongoni mwao.
“Unajua
hakuna mtu aliyaamini kuwa matukio ya kutisha yametokea Tanzania kwenye kisiwa cha amani, tunapaswa kuomba
rehema ili kujenga hofu ya kutenda mabaya,” alisema.
Mchungaji wa kanisa la Pentecostal
Assemblies of God (PAG) Yombo vituka
Stanley Ulomi akizungumza na mwandishi wa habari Mispa Charles.
Alisema Kanisa limekosa nafasi ya kusimama, wakiwamo Maaskofu, Wachungaji na watumishi wengine kusema ili kwa pamoja watu watubu na kumrejea mungu ili mabaya yasitupate.
Aidha, Ulomi alisema kuwa huwezi ukafurahia kuzima moto badala ya kuzuia, kuzima moto ni kazi ngumu na inapaswa kijikana nafsi bila woga.
Alisema kutokana na ukweli huo wa kujikana kanisa lake la PAG limedhamiria kufanya matamasha na makongamano kwa ajili ya kuiombea Tanzania ili kutokomeza uhalifu .
Wanatajia kufanya maombi ambayo yatawezesha matamasha hayo ili kila atakayeshiri mungu aweze kumwona mungu akitembea katika maisha yake.
Comments
Post a Comment