BONDIA ALIYENYIMWA VIZA KAANDAA PAMBANO.
Bondia Shaban Madilu kushoto wa Mtaa
wa Mbondole Kata ya Msongola anatarajia
kupanda ulingoni Kesho kupambana na Bondia Kutoka mkoani Tanga Patrick Kimweri.
Leonce
Zimbandu
MBONDIA Shaban Madilu wa Mtaa wa Mbondole Manispaa ya
Ilala ameamua kuandaa pambano la ngumi la raundi 10 la baada ya kunyimwa
visa ya miezi sita kwenda nchini
Uingereza.
Lengo la
Bondia huyo kuandaa pambano hilo ni kuukaribisha mwaka 2018 na kujitanga kuwa bado yupo kwenye ulingo wa
masumbwi hiyo anahitaji serikali kumsaidia ili kuondokana na ukiritiba.
Madilu
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
leo wakati wa kupima uzito kwa ajili ya pambano la kesho mwaka mpya kati
yake na Bondia kutoka Tanga Patick Kimweri.
Anasema baada ya kukosa visa hiyo hakukata tamaa,
hivyo aliendelea na mazoezi hadi kufikia wakati huu wa kuandaa pambano lake
mwenyewe ili serikali itambue kuwa hata pembezoni ya Jiji wapo wanamichezo.
Bondia Shaban Madilu na Bondia mwenzake Kutoka mkoani Tanga Patrick Kimweri
wakionesha namna ya pambano la kesho (mwaka mpya) litakavyokuwa na ushindani.
Alisema amewahi kushiri mapambano 28, matano ameshindwa, matano ametoka suluhu na yaliyobaki ameshinda hivyo anaendelea kuomba wadau kujitokeza ili kumpatia hamasa.
Patrick Kimweri alisema kuwa yeye amesafiri kuja Dar es Salaam kutafuta ushindi hata kama mpinzani wake amejiandaa lakini yeye amejiandaa na kujipanga kwa ushindi.
“Najua kesho lazima nitaaibuka na ushindi ili kurudi nao Tanga,” alisema.
Mratibu wa pambano hilo Mrisho Jogoo alisema kuwa haijawahi kutokea katika eneo hilo la Mbondole kuandaa pambano kama hilo, hivyo wananchi na wadau wa michezo wanapaswa kujitokeza kwa wingi.
“Naomba watu wajitokeze kuangalia mpambano mkali wa Mwaka mpya ambao utafanyika Mbondole Magengeni karibu na ofisi za serikali za mtaa,” alisema.
Comments
Post a Comment