MSIGWA ASEMA KINACHOLITAFUNA TAIFA NA BAADHI YA WASOMI.


Na Mwandishi Wetu, Iringa

CHAMA cha demokrasia na maendeleo chadema kimesema kuwa kinachotafuna Taifa la Tanzania ni baadhi ya wasomi na wanazuoni kutofanya kazi yao ipasavyo  ikiwamo kufanya tafiti na badala yake wanasubiri uteuzi wa kuwa viongozi kwenye nyanja mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa jana na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na pia Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Peter Msigwa wakati akizungumza na wanahabari mjini Iringa.

Msigwa amesema  katika Taifa kuna Maprofesa ambao wao ndio jicho la Taifa,wanafanya (Reseach) tafiti mbalimbali ikiwamo uchumi na kuwapa wanasiasa kwamba wakienda njia fulani taifa litafanikiwa lakini badala ya kufanya hivyo wamegeuka na kusubiri uteuzi na mambo yanapoharibika wanakaa kimya.


 “Hili nalo ni janga la Taifa tuna wasomi ambao wamekubali kuongozwa na vipofu,haiwezekani kipofu awe anaongoza wakati mwenye macho anaona hata kwenye Biblia inasema kipofu anaweza kumuongoza anayeona,hivyo   wasomi walitakiwa kuwa dira lakini kwasababu wao wanapenda kuteuliwa basi usomi wao wameweka mfukoni.”alisema Msigwa na kuongeza:

“Ukiwa Profesa, Phd holder, Shahada ukawa matendo yako unafanya sawa na mtu ambaye hajasoma huo usomi wako hauna maana.”alisema Msigwa.

 Msigwa aliwataka wasomi wa nchi hii kuinuka na kuacha kulipa aibu Taifa,wapo wachache sana wanaosema ikiwamo Profesa Mpangala,Baregu wengine wote wamekaa kimya.

Alisema kuwa hiyo ni aibu kwa Taasisi za kisomi nchini,wanatia aibu,kwa sababu wamekaa kimya wakisubiri uteuzi yaani Taifa limeingiza fedha nyingi lakini usomi wao hawautumii kama inavyotakiwa.

Katika hatua nyingine Msigwa amesema kuwa hivi karibuni amepigiwa simu na baadhi ya watu wakijaribu kumwambia yeye na baadhi ya wabunge wengine wa chadema kwamba 2020 hawatarudi kwenye majimbo yao na badala yake wajiunge na chama cha mapinduzi (CCM) na baadhi ya wananchi wamekuwa na maswali mengi kama atagombea ama laa.

 Alisema “Taifa hili ni kubwa kuliko mtu mmoja binafsi kurudi mimi kugombea au kushinda ubunge sio ishu,mimi sitakuwa mbunge wa milele katika jimbo la Iringa ,ishu hapa ni kusimamia misingi katiba bora tuweke sheria ambayo kila mtu hatakuwa juu ya sheria.”alisema Msigwa.

Alisema kuwa “bado hajakata tamaa nigombea mpaka kieleweke kama chama change kitanipitisha hiyo nitapambana nayo hainirudishi nyuma na hata juzi tumesimamisha uchaguzi kwa sababu wananchi wasio na hatia wamevunjwa miguu,nyumba kuvunjwa sasa kwa viongozi hatutaki kupata uongozi kwa gharama za damu za watu kwa sababu wenzetu wamefikia mahali hawataki kujenga hoja na badala yake wanatumia nguvu.”alisema Msigwa.

 Alisema kuwa ccm wameshindwa kujenga hoja ya kuwashawishi wananchi,wanatumia mabavu lakwanza kwenye level ya kisiasa chadema wamewashinda,ndio maana walisema badala ya kuendelea kuumiza wananchi wake waliwaambia tume ya uchaguzi Nec wakae meza moja na kuwaeleza kasoro zilizojitokeza wakati wa uchaguzi wa kata 43 hawataki na kusema kuwa uchaguzi ulikuwa wa haki.



Alisema kuwa kama chama wanajipanga kuangalia ni namna gani 2020 watatumia ushawishi gani kwa wananchi ili kupata kura lakini sio kama ccm ambao wanatumia nguvu.

Wakati huo huo Msigwa alizungumzia baadhi ya viongozi wa Chadema kuhamia  Chama Cha Mapinduzi (CCM)  hivi karibuni kumezuka mwenendo wa Madiwani na baadhi ya madiwani kuhamia CCM.

“Kikatiba ni haki kabisa,lakini kibinadamu mtu ambaye ana maadili baada ya kuchaguliwa na wananchi kuhama chama na kuhamia chama kingine lazima uwe na sababu za msingi  za kuwaridhisha wananchi  vinginevyo jamii itawapuuza.”alisema Msigwa

Alisema kuwa wamefikia kwa viongozi muda wowote kuhama bila ya kuwa na sababu ya msingi na kuongeza kuwa ni wakati mwafaka kwanza vyama vya siasa kupima watu wanaohamia chama kingine wanafaa au wanasukumwa na itikadi au.

Comments

Popular posts from this blog

ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.

NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

BONANZA LA BAJAJ, BODABODA LAFANA DAR