BUSTANI YA WAZEE YA UPENDO YAZINDULIWA.


 Baadhi ya viongozi wa serikali waliohudhuria kwenye uzinduzi  wa Bustani ya Upendo  wakishiriki mazoezi ya viungo  na baadhi ya wazee wa Mtaa wa Sea View jana jioni jijini Dar es Salaam.


 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Sea View Victor Muneni aliyevaa tisheti jeupe akizungumza na wazee wa Mtaa huo baada ya uzinduzi wa Bustani ya Upendo  iliyozinduliwa jana jijini Dar es Salaam.
 Wazee waliohudhuria uzinduzi huo wakijifunza juu ya matumizi ya mimea ambayo  inatumika kama mapambo na pia  inatumika kama  dawa ya kutibu magonjwa mbalimbali ikiwamo Alovera.

 Viongozi waliohudhuria uzinduzi huo akiwamo Diwani wa Kata ya Kivukoni Henry Massaba, wakiendelea kujifunza matumizi ya mimea ambayo inatumika kama mapambo na pia kama dawa.

 Picha ya pamoja ya wazee wa Mtaa wa Sea View pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa Bustani hiyo jana.
  Afisa Tarafa Kariakoo, Christina Kalekezi ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo akizungumza na wazee hao (hawapo pichani) baada ya kuzindua  Bustani hiyo jana, kulia ni Diwani wa Kata ya Kivukoni Henry Massaba. 

 Wazee wakiendelea kuelimishwa faida za mimea ambayo hutumika kama mapambo na pia ni  dawa zinazotibu  magonjwa mbalimbali.
Na Enles Mbegalo

MTAALAMU wa Saikolojia Zinat Fazal  ameitaka jamii kuto wanyanyapaa wazee bali iwapende ili wajifunze mambo mazuri kutoka kwao.

Hayo ameyasema jana jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa Bustani ya Upendo  itakayotumika  kufanyia mazoezi  kwa wazee wote wa Mtaa wa Sea view kila siku ya Jumamosi.

“Wazee wana dhamani tuwajali na tuwaheshimu kwani wao ndio wametufikisha sisi hapa tulipo jamii inatakiwa isiwanyanyapae bali iwapende kwani watajifunza mambo mengi mazuri kutoka kwao,”alisema na kuongeza

“Sisi wakati mwingine tunawadharau wazee kutokana na uzee wao ila tunatakiwa kuwapa kipaumbele kwa kuwapenda na kuwaheshimu,”.

Fazal alisema lengo la kuanzisha bustani hiyo ni kuelimisha jamii kwamba wazee wana thamani ,wajaliwe,wapewe upendo na heshima.


Naye Afisa Tarafa Kariakoo, Christina Kalekezi ambaye alikuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo  alimpongeza Mtaalamu wa  Saikolojia Fazal kwa ubunifu huo  ambao utawasaidia wazee wote wa Mtaa wa Sea View  kufanya mazoezi kila siku ya jumamos ili kuimarisha viungo vyao.

 “Niwaombe wazee wangu tusaidiane kukielimisha kizazi cha sasa hivi kwani kimepoteza kabisa dira ya utunzaji wa mazingira wakija hapa watajifunza mambo mengi kutoka kwenu,”


Pia alimpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea View Victor Muneni  kwa kushirikiana  na Mtaalamu wa  Saikolojia Zinat Fazal kwa kuweza kushauriana na kubuni Bustani hiyo ya Upendo

Comments

Popular posts from this blog

ASKOFU MWAMAKULA AMUWEKA WAKFU ASKOFU MPYA KENYA.

NABII ELIYA AZIDI KUFUNGUA WATU WALIOFUNGWA WENYE VIFUNGO MBALIMBALI.

RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN AZUNGUMZA NA MFALME WA DUBAI, WAFANYABIASHARA, ATEMBELEA BANDARI WA JEBEL ALI PORT NA KUTEMBELEA MRADI WA AKHEEL