JIJI LA DAR ES SALAAM NI MIONGONI MWA MAJIJI 10 YALIYOPATA TUZO YA C40 BLOOMBERG PHILANTROPIES 2017 CHICAGO NCHINI MAREKANI.
Mstahiki
Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akitoa neno la shukrani baada ya
kukabidhiwa tuzo ya C40 Bloomberge Philantropies .
Mstahiki Meya wa jiji la
Dar es Salaam Isaya Mwita katika akiwa kwenye mazungumzo ya pamoja na baadhi ya viongozi Chicago Nchini Marekani.
Mstahiki Meya wa jiji la
Dar es Salaam Isaya Mwita wa pili kushoto akiwa kwenye picha
ya pamoja na viongozi wengine Chicago Nchini Marekani.
Mstahiki Meya wa jiji la
Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto mstari wa mbele akiwa kwenye picha
ya pamoja na viongozi wengine Chicago Nchini Marekani wakiwa wameshika
tuzo zao.
JIJI
la Dar es Salaam ni miongoni mwa majiji 10 duniani ambayo yamepata tuzo
ya C40 Bloomberg Philantropies 2017 kupitia Mradi wa Mabasi
Yaendayo Haraka.
Katika tuzo hiyo mwaka huu imepokelewa na Mstahiki Meya wa
jiji la Dar es Salaam Isaya Miwta aliyerejea nchini alfajiri ya Desemba 8 mwaka
huu.
Jiji la Dar es Salaam limechangia tuzo hiyo na Jiji la New
York nchini Marekani na .
Mradi wa Mabasi yaendayo haraka unawahudumia abiria 200,000 kila
siku kwa kutumia mabasi ya kisasa ambayo yanachangia kupunguza msongamano wa
magari barabarani na kupunguza uchafuzi wa hali ya hewa na hivyo kuwa siri ya
mafanikio ya tuzo jijini hapa.
Tuzo ya C40 Bloomberg Philanthropies hutolewa kila mwaka
katika miradi inayotekelezwa kwenye maeneo mahususi matano ili kutambua
jitihada za majiji wanachama wa Taasisi ya mtandao wa Majiji zaidi ya 90
duniani inayoshughulika na namna bora ya kukabiliana na Athari za mabadiliko ya
Tabia ya Nchi Duniani.
Imetolewa
leo Desemba 10
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa
jiji.




Comments
Post a Comment