KANISA LA PENTEKOSTE LIMEZIPONGEZA TAASISI ZINAZOSAIDIA WATOTO WANAOISHI MAZINGIRA HATARISHI.
Emanuel kwaya toka Kanisa la Anglikana parish
ya Ukonga Mazizini wakitumbuiza kwenye
tamasha la kuchangia watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu hivi karibuni.
Mzee Kiongozi wa Kanisa la Pentekoste Tanzania
Parish ya Airport, Joel Ndutu akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo
Pichani) baada ya tamasha la kuchangia watoto wamaosihi kwenye mazingira
magumu.
Mkurugenzi wa
Taasisi ya Mkusikilize Msaidie Anaweza (MMA), Raphael Mwazyunga
alizungumza na waandishi wa habari Hawapo pichani baada ya kufanikisha tamasha
la watoto hao hivi karibuni katika Kanisa la Pentekoste Tanzania Parish ya
Uwanja wa ndege.
Na Leonce
Zimbandu
KANISA la
Pentekoste Tanzania Parish ya Uwanja wa Ndege imeipongeza Taasisi inayowasaidia watoto wanaoishi kwenye
mazingira hatarishi wakiwamo waliotelekezwa na wazazi na jamii.
Pongezi hizo
zimetolewa na Mzee Kiongozi wa Kanisa hilo, Joel Ndutu baada kufanyika kwa
tamasha lililohusisha wadau ambao
walichangia vitu ili kuhakikisha
wapelekwa shule mwakani.
Ndutu
aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliofika kwenye
tamasha na kushuhudia tukio hilo lililofanyika katika Kanisa hilo hivi
karibuni.
Alisema
taasisi imefungua milango ya watu kutambua athari za kutelekeza watoto na matokeo
yake watoto kuishi maisha hatarishi ambayo hayampendezi mungu.
“Kanisa
tumefurahi kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Msikilize Msaidie Anaweza kufanya
tamasha hilo katika kanisa hilo, hiyo ni hatua moja ya kuunga mkono juhudi za
serikali,” alisema.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Msikilize Msaidie Anaweza (MMA), Raphael Mwazyunga alisema lengo
la kuanzisha taasisi hiyo ni kuwasaidia watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu na hatarishi.
Alisema
walianza kuingia mitaa na kufanikisha
kuwapata watoto 70 kati yao 36
wanaishi katika mazingira hatarishi lakini wengine wanaishi na mzazi
mmoja wa kike ambaye hawezi kujikimu
kimaisha.
“Chanzo cha kutelekeza watoto mitaani kinatokana na kusambaratika kwa ndoa, hivyo wanawake
wanapaswa kupunguza hasira ili kulinda ndoa zao,” alisema.
Alisema
ataendelea kushirikiana na harakati za kuunga mkono juhudi za Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam, Paul Makonda kuwachukulia hatua wanaume watakatelekeza watoto.
Comments
Post a Comment