MADIWANI ILALA WAOMBA TARULA IVUNJWE IMESHINDWA KUTENGENEZA BARABARA.
Na
Heri Shaaban
BARAZA la Madiwani manispaa
ya Ilala imesema kuwa imeshindwa kufanya kazi na Wakala wa Barabara
Tarula kwa kuwa toka wapewe jukumu na Serikali hadi leo amna barabara
zilizojengwa na kupelekea kero kwa wananchi.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam
jana katika kikao cha Baraza la Madiwani Ilala na Mwenyekiti wa Baraza hilo
Naibu Kaimu Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto.
Akizungumza katika baraza
hilo Kumbilamoto alisema toka Serikali iwape mamlaka Tarula hadi leo amna
barabara zilizojengwa ndani ya manispaa hiyo na kupelekea kero kubwa ikiwemo
Barabara za Vingunguti ambapo kwa sasa magari yanashindwa kupita kutokana na
kuwa na mashimo makubwa.
" Mimi kama Mwenyekiti
wa kikao cha baraza la leo tumeshindwa kufanya kazi na Tarula kwani imekuwa
jina tuu na kama kweli wapo basi Serikali iwape fedha iweze
kujenga Barabara za Halmashauri ambapo nyingi zimeharibika"alisema
Kumbilamoto.
Alisema ndani ya
Manispaa ya Ilala kwa sasa vilio vikubwa ubovu wa barabara za wananchi ndio
kero kubwa na madiwani hawana uwezo wa kutatua kero katika kata zao
Kutokana na posho zao nyingi kufutwa kubaki na mshahara ambao wanalipwa kila
mwezi.
Akielezea kuhusu madiwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kususa kikao cha baraza hilo na
kutoka nje ya ukumbi wakiongozwa na Diwani wa Tabata Patrick Asenga.
Kumbilamoto
alisema walitaka kufahamu mazimio ya kikao kilichopita cha madiwani
na agenda ya yatokanayo katika Muhtasari ilikuwa hawakuweka katika
kabrasha hilo.
Alisema baadhi
ya mambo mengine ambayo walitaka kuuliza yatokanayo ni swali alilouliza Diwani
wa Kata ya Kipawa Kennedy Saimoni kutaka kujua matumizi ya fedha Mfuko wa Jimbo
la Segerea hata hivyo alikupata majibu.
Kwa upande wa Diwani wa Viti
Maalum Ilala Saada Mandangwa(CCM) katika baraza hilo aliwanyima nafasi Madiwani
wa CHADEMA waliokuwa wakitaka kumburuza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala
Palela Msongole wakati Mkurugenzi alishaomba msamaha makosa hayatajirudia tena
katika vikao vingine.
Naye Diwani wa Kata ya Ilala Saddy Kimji ameomba Serikali iwalete Tarula kama
kweli Wapo waweze kushiriki Vikao vya baraza la madiwani Ilala na
kufahamu changamoto zilizopo za barabara za halmashauri.
Diwani Saddy alisema ni aibu
ndani ya manispaa yao ambayo IPO Jirani na sura ya nchi yaani IKULU lakini
barabara mbovu.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya
Ilala Dkt.Victoria Ludovick alisema Manispaa inatenga fedha katika bajeti ijayo ili kila kata waweze kutoa matibabu kwa wananchi bure .
Comments
Post a Comment