MEYA MWITA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAJUMBE KUTOKA KISIWA CHA MAYOTTE.
Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda
wa Mayotte Nchini Ufaransa, kulia Hamidani Magoma akimuelekeza jambo kwenye
kwenye dokomenti Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
walipomtembelea ofisini kwake na kujadili mambo mbalimbali ya maendeleo katika
sekta ya biashara jijini hapa.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa kwanza kushoto, akimsikiliza Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda Hamidani Magoma mwenyemiwani walipokutana katika ofisi za Mastahiki Meya jiji.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Saalam Isaya Mwita
akimkabidhi Rais wa Shirikisho la wafanyabishara na Viwanda wa Mayotte
Hamidani Magoma Kamusi ya Kiswahili baada ya kuzungumza Kiswahili.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
watatu kulia mstari wa mbele akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe kutoka
Kisiwa Cha Mayotte kilichopo Nchini Ufaransa walipomtembelea ofisini kwake.
MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita
amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa watu 10 kutoka Kisiwa cha Mayotte
kilichopo Nchini Ufaransa.
Ujumbe huo ulikuwa umeambatana na wabunge watatu
kutoka Nchini humo, Rais wa Shirikisho la wafanyabiashara wa Mayotte pamoja na
wajumbe wengine ambao ni wawakilishi kutoka kampuni mbalimbali kisiwani humo.
Katika mazungumzo hayo, Mstahiki Meya Mwita na wageni
wake wamejadili mambo mbalimbali ya maendeleo jijini hapa hususani masuala ya
kibiashara ambapo amewakaribisha na kuahidi ushirikiano kwao.
Aidha Meya Mwita pia ameshangaa kuona ugeni huo
kutoka Kisiwa cha Mayotte wakizungumza Kiswahili jambo ambalo alidai kuwa ni la
kihistoria kutokana na historia ya Nchi hiyo.
Kutokana mshangao huo, ambao uliambatana na furaha
ndani yake, aliwakabidhi zawadi ya Kamusi ya Kiswahili kwa lengo la kuendelea
kujifunza zaidi Lugha ya Kiswahili pindi watakaporejea nchini kwao.
“ Nimefarijika na kushangaa baada ya kusikia
asilimia 40 ya wananchi wakisiwa cha Mayote wanazungumza lugha ya Kiswahili,
hii ni ajabu, lakini inaonyesha ninamna gani ambavyo watu wanaipenda Lugha
yetu” amesema Meya Mwita.
Awali jumbe huo ulikutana na kufanya mazungumzo na
Shirikisho la wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo Tanzania.
Imetolewa
leo Desemba 2 na Christina Mwagala, Afisa habari Ofisi ya Meya wa jiji.




Comments
Post a Comment