MWENYEKITI AWATAKA WAKAZI WA MJI MPYA KUSIMAMISHA UJENZI MPYA.
Na Mwandishi Wetu.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Mtongani Kata ya
Kunduchi Richard Rusisye amewataka wakazi wa Mji Mpya kuacha kuendeleza
ujenzi holela wasubiri utaratibu kutoka
kwa Maofisa wa Mipango Miji ili waweze
kujenga makazi bora.
Hayo aliyasema jijini Dar es Salaam hivi
karibuni Mwenyekiti wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa
habari kuhusu changamoto mbalimbali zilizopo kwenye mtaa wake.
Mwenyekiti Richard Rusisye alisema changamoto kwenye mtaa wa Mtongani
ni ujenzi holela hasa Mtaa wa Mji
Mpya ambapo wakazi wa maeneo hayo wamekuwa wakijenga nyumba mpya bila kufuata
utaratibu wa Mipango Miji.
“Wakazi wa eneo la Mji Mpya wasimamishe ujenzi mpya
wa nyumba ili kutoa fursa ya kutoa picha ya Mtaa huo kwa Maofisa wa Mipango Miji hadi pale watakapokuja kupima maeneo hayo, kwani utaratibu unafanyika
ili kuja kupanga vema Mtaa huu,”alisema
Pamoja na Mwenyekiti Richard Rusisye kutoa agizo hilo la ujenzi mpya kusimamishwa lakini bado
wakazi wa eneo hilo wameendelea na ujenzi.
Hata hivyo Mwenyekiti Richard Rusisye alizungumzia suala la usafi wa Mazingira katika mtaa wake alisema mtu yeyote asiyefanya
usafi atatozwa faini ya Shilingi 50,000.
“Mtu yeyote asiyefanya usafi wa mazingira atalipa
faini ya Shilingi 50,000 na Askari wangu wa Ulinzi Shirikishi wanazungukia
mitaani kwaajili ya kudhibiti usafi wa mazingira atakayebainika kwa hili
hatutakuwa na huruma naye,”alisema Mwenyekiti.
Hata hivyo Mwenyekiti huyo alizungumzia changamoto
mbalimbali zilizopo kwenye mtaa wake ikiwamo Ulinzi Shirikishi ambapo
wamejipanga kuboresha ili kupunguza wizi mdogo mdogo uliopo kwenye mtaa.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Mtongani Kata ya
Kunduchi Richard Rusisye , akimuingia mmoja wa wafanyabiashara wa ndizi na viazi eneo la Mji Meko ambako Serikali ya Mtaa ilitoa eneo hilo la wazi kwaajili ya fursa kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Mtongani Kata ya
Kunduchi Richard Rusisye akiendelea kumuonyesha Mwandishi wa Habari maeneo ambayo Serikali ya Mtaa imetoa kwaajili ya wafanyabiashara wadogo wadogo.
Comments
Post a Comment