MWENYEKITI WA CCM ALITUPIA LAWAMA JESHI LA POLISI.
Mfanyakazi wa Mk Guest, Josephine Simon alionesha majera
aliyofinywa na wanaodaiwa kuwa ni askari polisi.
Mwenyekiti wa CCM
Kata ya Kiwalani, Mathias Kahinga akizungumza na wanahabari hawapo
pichani baada ya kuzungumza na mkuu wa polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni jana
jijini Dar es Salaam.
Leonce
Zimbandu
MWENYEKITI
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya
Kiwalani,Mathias Kahinga amelitupia lawama Jeshi la Polisi nchini kwa kutumia silaha kuwakamata wateja wanne na
mfanyakazi mmoja wa kike.
Novemba 27, 2017 askari 10 waliovaa kiraia
walifika katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo MK guest iliyopo Mtaa wa
Kigilagila wakiwa na silaha za moto kwa kuwakamata na wengine kufinywa.
Kahinga aliyasema
hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuonana na Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni jijini Dar es Salaam jana.
Alisema
hakubaliani na kitendo cha kihuni kilichofanywa na askari hao kwa vile yeye ni
kiongozi wa Kata anawajibu wa kusimamia serikali katika eneo hilo, hivyo
alipaswa kuelezwa tatizo baada ya ukamataji huo.
“Inashangazwa
eneo langu la biashara linavamiwa askari bila taarifa na kuwafanya wageni wengi
kuhama, hali hiyo inafanya biashara kuwa ngumu kwa hofu ya kukamatwa,” alisema.
Mikidadi
Mohamed ni mmoja wa wageni waliokamatwa alisema kuwa yeye alikamawa wakati
akitoka chumbani kwenda nje na kukutana na askari hao na kumkamata.
Alisema
alipojaribu kuuliza kosa lake la kukamatwa ni nini, walimjibu kuwa atajuulisha
baada ya kufika katika kituo kidogo cha polisi cha Yombo Mama.
“Nimeshangaa
hata nilipofikishwa katika kituo hicho sikuelezwa kosa bali waliniweka ndani
kwa saa mbili na kasha kunipeleka kituo cha Buguruni na kutolewa jioni kwa
faini,” alisema.
Mfanyakazi
wa usafi wa guest hiyo, Josephine Simon alisema kuwa yeye ameshangazwa na
kudhalilishwa na askari wa kiume kwa kunifinya na kuniachia majeraha kwenye
mwili wangu.
Alisema hakufurahishwa na kitendo cha askari hao
kufika na kuanza kuwakamata wateja
waliofikia katika nyumba ya kulala wageni.
“Unajua
waliniburuza kutoka ndani ya guest hadi kwenye gari, huku wengine wakinifinya
kwenye mikono yangu na kuniachia alama hadi sasa,” alisema.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema kuwa Jeshi hilo limepokea
malalamiko hayo na wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kama taratibu
zilikiukwa.
“Tukithibitisha
kama taratibu hazikufuatwa askari waliohusika watachukuliwa hatua lakini askari
yeyote anaruhusiwa kutekelezwa wajibu wake kwa mujibu wa sheria,” alisema.
Comments
Post a Comment