MWITIKIO MDOGO WA MIKUTANO UNAVYOKWAMISHA ULINZI NA USALAMA KWENYE MITAA.
Na Mwandishi
Wetu.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Salasala Kata ya
Wazo Hashim Semboja amesema mwitikio mdogo wa wananchi kwenye vikao vya mitaa
kunachangia kutotatuliwa kwa tatizo la Ulinzi Shirikishi.
Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza
na mwandishi wa habari ofisini kwake juu ya changamoto mbalimbali zilizopo kwenye mtaa wake ambapo alisema changamoto
kubwa ni Ulinzi na Usalama.
“Tangu tuingie madarakani tumekutana na changamoto
moja kubwa ya Ulinzi na Usalama ambapo kuna matukio mengi ya wizi yalikuwa
yanatokea ikiwamo ya watu kuibiwa kwenye
Baa zao pamoja na kuuawa kwa risasi,” alisema na kuongeza
“ Lakini ukiitisha mkutano wananchi
hawaipi uzito na tumefanya
mikutano sita ya Ulinzi na Usalama kwa
kila zone ila muitikio ni mdogo sana pia
itikadi za vyama vya siasa zinachangia
pia wananchi kutounga mkono Ulinzi na Usalama,”
Hata hivyo Semboja alisema pamoja na changamoto hizo wamefanikiwa kupata fedha kutoka kwa wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo zaidi ya Shilingi Milioni 5, 000,000 kwaajili ya kuendeleza ujenzi wa Kituo cha Polisi ili kuimarisha zaidi usalama kwenye mtaa huo.
Pia alisema Ofisi ya Mbunge wa Kawe Halima Mdee itachangia Shilingi Milioni 10,000,000 kwaajili ya kuenzeka kituo hicho.
Semboja aliwashukuru wananchi pamoja na wadau mbalimbali wapenda maendeleo walioweza kuchangia fedha hizo kwaajili ya kumalizia kituo hicho ambapo kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye mtaa wao.
Comments
Post a Comment