*RC MAKONDA ATANGAZA DISCOUNT YA 20% HADI 70% KWA WANANCHI WOTE WATAKAOFIKA MADUKA YA MLIMANI CITY*.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
*Mhe. PAUL MAKONDA* ametangaza Punguzo la Bei *(Discount) la 70%* kwa Bidhaa
zote zinazopatikana Ndani ya *Maduka Mlimani City* kwa muda wa *Wiki moja
kuanzia Leo.*
Punguzo hilo la bei ni kwa
*Wananchi Wote* ikiwa ni zawadi ya *RC MAKONDA* Kuelekea Sikukuu za *Christmas
na Mwaka Mpya* ili kuwapunguzia wananchi makali ya Gharama.
*RC MAKONDA* amesema hayo
kwenye Hafla ya kuwakaribisha wanafunzi wa Vyuo vikuu Mwaka wa Kwanza *DAR
FRESHERS PARTY 2017* ambapo amesema tamasha hilo litakuwa likifanyika *kila
Mwaka* kwa kushirikisha *Wasanii wakubwa kutoka Ndani na Nje ya Nchi.*
Ameshukuru Vyombo mbalimbali
vya habari ikiwemo *TBC, E. FM na E TV pamoja na Channel Ten* kwa kufanikisha
Tamasha hilo.
Aidha amewashukuru wasanii
mbalimbali wakiwemo *WCB, AY, FID Q, RUBY, KASSIM MGANGA, MWANA FA,
RAY C, LADY JAYDEE, MSAMI, CHRISTIAN BELLA, DULY SYKES na MRISHO MPOTO* kwa
kujitolea kutoa Burudani bila Malipo.
Amesema *Lengo la Tamasha
hilo ni kujenga umoja kwa kuwakutanisha wanafunzi wa Vyuo mbalimbali
kubadilishana mawazo na kupatiwa maarifa.*

Comments
Post a Comment