RC MAKONDA ATOA RUNINGA 69 KWA MAGEREZA NA HOSPITAL ZA DAR ES SALAAM.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiwa amesimama katika Runinga za kisasa 69 (Flat Screen) Touch zenye ukubwa wa Inch 40 aambazo amezitoa Magereza
na Hospital zote za Dar es Salaam kuwezesha wafungwa na wagonjwa kupata haki ya
kikatiba ya kupata Habari.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makond akiwa ameshika moja ya Runinga ambazo amezitoa msaada leo kwenye Magereza na Hospital zote za Dar es Salaam.
Mkoa
wa Dar es Salaam umeadhimisha Siku ya Uhuru kwa Kuwatembelea Wafungwa na
Maabusu kisha kupata Chakula cha Pamoja na kutoa huduma ya Masaada wa Kisheria
na Ushauri na Saha kwa Wafungwa na Mahabusu.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA ametoa msaada wa Runinga za kisasa
69 (Flat Screen) Touch zenye ukubwa wa Inch 40 kwa Magereza na Hospital
zote za Dar es Salaam kuwezesha wafungwa na wagonjwa kupata haki ya kikatiba ya
kupata Habari.
Hii ni Historia kwa Dar es
salaam kuwa Mkoa wa kipekee wenye Runinga Magerezani zinazowawezesha Wafungwa
na Mahabusu kupata Habari na Hotuba za Rais ili kuwapunguzia msongo wa mawazo
ili wasiwe na mawazo ya kujiua ambapo zitagawanywa kwenye Magereza ya Segerea,
Keko na Ukonga.
Baadhi ya viongozi wa Dini walioongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwaajili ya kufanya Dua na Sala pamoja na kuwafariji wafungwa hao.
RC MAKONDA aliongozana na Viongozi wa Dini waliowafariji wafungwa na kuwafanyia Sala na Dua huku watu wa Ustawi wa Jamii wakitoa msaada wa ushauri na saha kwa wafungwa.
MAKONDA ambae amepokelewa kwa furaha kubwana wafungwa wa Gereza hilo amewasihi kutokata tama kwa kuwa bado wanayo nafasi ya kutimiza ndoto zao baada ya kumaliza kifungo ambapo amewahimiza kuwa mabalozi wazuri kwa jamii.
Ili kupunguza msongamano wa Mahabusu Gerezani RC MAKONDA amesaidia zaidi ya Mahabusu na Wafungwa 200 wa Gereza la Segerea kupata msaada wa sheria ambao walikuwa hawana uwezo kifedha.
Aidha MAKONDA ametoa Magodoro 100, Vifaa vya Usafi na Sabuni za Kuoga na Kufua kwa Wafungwa na Mahabusu.
Baadhi ya Maabusu na Wafungwa wamemshukuru RC MAKONDA kwa kuwa kiongozi wa Kwanza na wa pekee aliewatembelea na kupata chakula cha pamoja, kuwapatia Runinga, kusikiliza changamoto zao na kuwapatia Wanasheria na watu wa Ustawi wa Jamii kitendo kilichowafariji.
Aidha Wameshukuru pia kitendo cha RC MAKONDA kusikiliza Changamoto zao na kuzipatia majibu ambapo wamemuahidi kuwa wamebadilika na watakuwa mabalozi wazuri kuhimiza jamii kuzingatia Sheria.







Comments
Post a Comment