WAISLAM WAMETAKIWA KUTOA USHIRIKIANO KWA WAFADHILI WANAOJENGA MISIKITI.
Na Ramadhani Kangale.
Waislam Nchini wametakiwa kutoa ushirikiano pale wanapofika
wafadhili wakujenga misikiti katika maeneo yao ili kuendeleza mbele uislamu.
Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na muakilishi wa
Taasisi ya Human Relief Fondation ya nchini Bahrain hapa Tanzania
Mbarak Fahmy wakati wa ziara waliyoifanya viongozi wa Taasisi hiyo kutembelea
miradi yao ya misikiti waliyo ijenga hapa Tanzania.
Fahmy alisema endepo kutakuwepo ushirikiano wa kutosha
baina ya waumini na wafadhili wanaojenga misikiti itakuwa rahis wafadhili
kutekeleza majukumu yao bila kujali umbali wa eneo lilo hitajika kujenga
misikiti au madrasa.
Alisema kuna baadhi ya waumini wadini wamekua wakimiliki maeneo makubwa lakini kutoa kwa ajili ya ALLAH wanaonatabu huku akilazimika kutembea umbali mrefu kwenda kufanya ibada.
Akizungumzia malengo ya Taasisi hiyo kwa hapa Tanzania wanakusudia kujenga kituo kikubwa cha watoto yatima hapa tanzania maeneo ya chanika na kigamboni pamoja na huduma zote za kijamii ikiwemo uchimbaji wa visima na ujenzi wa misikiti na madrasa.
Alisema lengo la kujenga kituo cha watoto yatima ni kuwaokoa watoto hao wasiingie katika makundi ambayo yasiyofaa na ni hatarishi.
Aliongeza kuwa kumekuwa na wimbi la watoto wa mitaani wengi wao wamepoteza wazazi wao na wengine kutelekezwa na wazazi au walezi hivo inakua aipendezi kuachwa wakizurula mitaani nilazima wachukulliwe wapewe elimu ili nawao waje kuwa watu wema na kujitambua nakua na familia zao katika kuliona hilo ndipo walipoweka mikakati ya kutaka kuanzisha vituo hivo.
Misikiti waliyotembelea viomgozi hao ni msikiti Li-lahi uliyopo Mbezi Malamba Mawili Wilayani Ubungo na msikiti wa AL-akswa uliyopo Zingiziwa Chanika Wilaya ya Ilala na kuwagawiwa sadaka ya nyama ya Ng'ombe.
Asalam alaykum am Hassan Hamadi Mwashughuli from Majengo mapya-Likoni -Mombasa ,Kenya am requesting assistance of construction of Masjid and Madhrasa to our Muslim community, the site is available , please assist the young Muslim to know their creator and have good start of their entire life here and.after , please assist us build our religion and our youths,.we hope nice feedback inshaAllah.
ReplyDeleteAsalam alaykum warahmatullah wabarakatuh.