WAKRISTO WASHAURIWA JINSI YA KUPELEKA MAOMBI MBELE ZA MUNGU.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter , akifungua watu waliofungwa katika vifungo mbalimbali ikiwamo magonjwa na shida mbalimbali jana katika semina ya Maombi iliyofanyika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa
Rev Joseph Marego iliyoanza jana 20 Desemba 2017 jijini Dar es Salaam.
Watu wakiendelea kufunguliwa katika vifungo mbalimbali na kupokea Unabii kwa Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life Eliya Peter, katika semina ya maombi inayoendelea katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa
Rev Joseph Marego.
Waumini wa Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego, walioshiriki semina ya Maombi iliyoanza jana.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter, akiendelea kuwaombea watu wenye shida mbalimbali walioshiriki kwenye semina hiyo, iliyofanyika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego.
Baadhi ya waumini walioshiriki semina hiyo jana katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego, iliyofunguliwa na Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter.
Baadhi ya waumini wakiendelea kufuatilia mafunzo ya semina hiyo ya Maombi inayofanyika katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego .
Baadhi ya waumini wakiendelea kufuatilia mafunzo ya semina hiyo iliyofanyika jana Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego.
Rev Joseph Marego wa Kanisa la Tabata Kimanga EAGT, akimkaribisha Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life Eliya Peter (hayupo pichani) kwaajili ya kufungua semina ya Maombi iliyoanza jana kwenye Kanisa hilo.
Mke wa Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life, Eliya Peter kushoto na kulia ni Mke wa Rev. Joseph Marego.
Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki, Eliya Peter , akiendelea kuwafungua watu waliofungwa kwenye vifungo mbalimbali.
Enles Mbegalo
ASILIMIA 70 ya Wakristo hawapeleki maombi mbele za
Mungu ila wanapeleka malalamiko.
Hayo yalisemwa na Mtumishi wa Mungu na Nabii wa Kanisa la Christian Life lililopo Tegeta Nyuki,
Eliya Peter wakati akifungua semina ya Maombi katika Kanisa la Tabata Kimanga EAGT kwa Rev Joseph Marego iliyoanza jana 20
Desemba 2017 jijini Dar es Salaam.
Alisema Wakristo kama wana wa Mungu huwasiliana na
Mungu kwa njia ya maombi kwa kuwa maombi ni njia pekee ya kufanya Mungu aseme
nao.
“Maombi ni njia pekee ya kupeleka hitaji lako mbele za Bwana ila
Wakristo hawapeleki maombi mbele za Mungu ila wanapeleka malalamiko,”alisema
Pia aliwataka Wakristo kutenga muda kwaajili ya
maombi kwani Maombi unayoombwa leo
yanaweza yakawa jambo la kumkumbusha Mungu hitaji lako la kesho.
“Kitabu
cha Wafilipi 4: 6….. Msijisumbue kwa
neno lolote, bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru,
Haja zenu na zijulikane na Mungu na
katika Kitabu cha 1 Wathesalonike 5: 17…..Ombeni bila kukoma,”.
Mtumishi wa Mungu
na Nabii Eliya Peter, aliwataka
Wakristo kuwa waombaji na sio kuombewa.
“Jifunze kuingia magotini wewe kama wewe tatizo la
watu wengi wanaomba lakini hawaamini
wanachoomba kama kitatokea, Kitabu
cha Marko 11: 24 ….Kwa sababu hiyo nawaambia Yoyote myaombayo mkisali, aminini
ya kwamba mnayapokea , nayo yatakuwa yenu,”
Comments
Post a Comment