WAZEE ZINGIZIWA WAOMBA RAIS AWAKUMBUKE.
Kamati
ya mipango na fedha Kikundi cha Wazee Amani Group wakimsikiliza mwalimu wa
ujasiliamali (Hayupo pichani) alipowatembelea hivi karibuni.
wa
Kikundi cha Wazee Amani Group wakimsikiliza mwalimu wa ujasiliamali (Hayupo
pichani) alipowatembelea hivi karibuni.
Wanakikundi
cha Wazee wa Amani Group wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo ya
ujasiliamali.
Leonce
Zimbandu.
KIKUNDI cha
Wazee Amani Group (WAG) kilichopo Kata ya Zingiziwa Manispaa ya Ilala,
kimemuomba Rais John Magufuli kuwakumbuka na kuwaita kwenye mikutano ya Wazee
wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Ombi hilo limetolewa
na wazee hao baada ya kufanya usajili kikundi chao mwaka 2002 kwa namba 337 na
kukabidhiwa cheti chenye kumb. namba
19238 kwa lengo la kutetea haki za wazee wa Tanzania, Afrika na Ulimwenguni
kote.
Mwenyekiti
wa kikundi cha WAG, Msahilo Mbegu aliyasema hayo alipokuwa akizungumza kwa uchungu
na waandishi wa habari waliowatembelea hivi karibuni ili kujua changamoto
zinazowakabili.
Alisema
haelewi utaratibu unaotumika kuwatambua wazee wa kukutana na Rais bila hata
kikundi chao ambacho kilichosajiliwa
kisheria kupata mwaliko wa kuhudhuria hata mtu mmoja.
“Tunaishukuru serikali kututambua rasmi kwa kuunda wizara inayotushughulikia matatizo yetu
lakini tunahitaji huduma za msingi zipatikane kwenye vituo vya afya,” alisema.
Alisema
wazee wanachangamoto nyingi, ikiwamo afya (bima), chakula na malazi kwa
vile wengine hawana watu wa kuwasaidia,
hivyo kikundi hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia wengine.
Aliongeza
kuwa iwapo serikali itawaunga mkono kwa kuwaunganisha na kikundi cha wazee
waliopo nchini Afrika ya Kusini
watafurahi ili wabadilishana nao uzoefu wa namna ya kuendesha vikundi hivyo.
Kufuatia
hatua hiyo iliyochukuliwa na wazee hao kukaa pamoja na kuunda umoja huo ni
jambo la kuwapongeza na serikali inapaswa kuongeza nguvu ili kuwapatia nyenzo
za kujikimu.
Comments
Post a Comment