WAZIRI LUKUVI MGENI RASMI MKUTANO WA WATAALAM WA ARDHI.
Na
Heri Shaaban
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Wiliam LUKUVI anatarajia kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa
mwaka wa Wataalam wa Ardhi wa Wataalam wa Ardhi waliowai kusoma Chuo cha Ardhi
Morogoro .
Akizungumza na waandishi wa
Habari Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Wataalam Waliowai kusoma Cha Ardhi
Morogoro, Salum Shaka ,alisema mkutano huo unatarajia kufanyika machi
2018 lengo la mkutano huo ni mwendelezo wa mikutano ya Umoja huo ambayo inafanyika
kila mwaka.
"Umoja wa Wataalam wa
Chuo cha Ardhi Morogoro tumeweka utaratibu kila mwisho wa mwaka kufanya
tathimini na kujadili Maendeleo ya Umoja wetu " alisema Shaka.
Salum alisema kongamano hilo
mwaka huu linatarajia kupambwa na WAZIRI mwenye dhamana Wiriam LUKUVI katika
viwanja vya vya Chuo hicho .
Aliwataka wataalam wote ambao waliwai kusoma Chuo hicho wajitokeze siku hiyo kuzungumza na WAZIRI wao katika viwanja vya Chuo.
" Siku hii ni maalum kwetu ambapo mwanzoni mwa machi 2018 tutakutana mambo mbali mbali ya Chuo yatajadiliwa kwa lengo la kupanua wigo wataalam kwa wataalam kujenga uwezo katika utendaji wa majukumu yao na kujenga weledi wakiwa kazini" alisema.
Alisema siku hiyo ni maalum kwa kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu sekta ya ardhi.
Aidha alisema kwa sasa nchi yetu inaelekea Tanzania ya Viwanda na kauli mbiu siku hiyo" Ardhi ni msingi Mkuu kufikia azima ya Tanzania ya Viwanda"


Comments
Post a Comment